Warsha kuhusu mitandao ya mawasiliano ya kijamii na nafasi yake katika kujenga uwelewa

Maoni katika picha
Kitengo cha maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya warsha kuhusu mitandao ya mawasiliano ya kijamii na nafasi yake katika kujenga uwelewa, watumishi wa vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu ndio washiriki wa warsha hiyo, nayo ni sehemu ya kujenga uwezo wa watumishi, wamepewa warsha hii kutokana na kuenea kwa matumizi ya mitandao hiyo katika jamii, halafu mitandao ina athari nzuri zenye manufaa na athari mbaya zenye madhara kwa mtumiaji au jamii.

Warsha ilikuwa na mada nyingi zinazo husu namna ya kuamiliana na mitandao ya mawasiliano ya kijamii, na njia muwafaka ya kutumia mitandao hiyo, tumeongea na mhadhiri wa warsha hiyo Ustadh Bashaar Tawiji amesema kuwa: “Warsha ilikuwa na anuani isemayo: (Kuongeza uwelewa wa kutumia mitandao ya mawasiliano ya kijamii), kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, lengo la warsha hii ni kuongeza uwelewa wa matumizi ya mitandao ya mawasiliano ya kijamii”.

Akabainisha kuwa: “Warsha imezungumzia namna ya kuamiliana na taarifa sahihi, na kuhakiki usahihi wa taarifa zinazo andikwa mitandaoni kwa (utambuzi wa mitambo ya mawasiliano) au kijulikanacho kwa jina la Khawarizamiyya na jinsi ya kuamiliana na waandishi, pamoja na jinsi ya kutambua mtumiaji wa facebook, wakati na maneno anayotumia, mwisho namna ya kunufaika na wingi wa mitandao ya mawasiliano ya kijamii”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: