Kukamilika kwa mradi wa jengo la wanafunzi wa kitivo cha tiba ya meno katika chuo kikuu cha Al-Ameed

Maoni katika picha
Kitengo cha majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya kimetangaza kukamilika mradi wa jengo la wanafunzi wa kitivo cha tiba ya meno katika chuo kikuu cha Al-Ameed, kilichopo kitongoji cha Saádiyya kwenye mkoa wa Karbala, limejengwa kwa umaridadi mkubwa na ufanisi wa hali ya juu kwani kitakuwa kituo cha mfano kwa wanafunzi wa chuo.

Hayo yamesemwa na Mhandisi mkazi na msimamizi wa mradi huo Karaar Barihi kutoka kitengo tajwa, akaongeza kuwa: “Mafundi wetu waliojenga mradi huo wamefanya kazi kubwa chini ya mkakati uliopangwa, jengo limefungwa mitambo ya kisasa ya umeme, kamera, mawasiliano, viyoyozi na alam za tahadhari, mambo yote yamesha kamilika na jengo liko tayali kupokea wanafunzi”.

Akafafanua kuwa jengo linaukubwa wa mita (420) na linaghorofa nne (tabaka la chini na ghorofa tatu zingine), tabaka la chini lina vyumba vitatu vya ofisi pamoja na ukumbi wa mapokezi, na ghorofa tatu zilizobaki kila moja inakumbi mbili na madarasa mawili, kila darasa lina nafasi ya wanafunzi (28) pamoja na sehemu ya vyoo na vyumba vingine vya kutolea huduma, baada ya kumaliza ujenzi wa jengo hilo tumeanza kutengeneza njia zinazo ingia eneo katika eneo hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: