Mgeni ametembelea makumbusho ya Alkafeel na ameangalia mali-kale na nakala-kale

Maoni katika picha
Mgeni kutoka Norwey (Yorin Bayorin) ametembelea makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuangalia maendeleo ya makumbusho hiyo katika upande wa utunzaji na uonyeshaji, akasikiliza maelezo kamili kuhusu mali-kale zilizopo ndani ya makumbusho, ameambiwa historia kwa ufupi ya kila mali-kale na njia za utunzwaji wake.

Bayorin amefurahishwa na mali-kale adimu alizoona kwenye makumbusho hiyo, kama vile aina tofauti za panga, miswala ya kifahari na nakala-kale, aidha amefurahishwa na aina ya upangaji wa vitu ndani ya makumbusho ambao umefanywa na watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wa kitengo cha makumbusho.

Mwisho wa ziara yake ametoa shukrani za dhati na kusema kuwa: “Nimekutana na viongozi katika makumbusho ya Atabatu Abbasiyya tukufu, napenda kutoa shukrani za dhati kutoka ndani ya moyo wangu kwa mapokezi mazuri na msaada wenu kwangu, natamani kuwatembelea tena mara nyingine”.

Kumbuka kuwa Bayorin ni muandishi na msemaji mkuu, naye ni mnorwey mwenye umri mdogo anaye tembea kila nchi duniani, na Iraq ndio nchi ya mwisho aliyotembelea, amefika kwenye mikoa (18) ukiwemo mkoa huu wa Karbala tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: