Maahadi ya Quráni tukufu inaendelea na semina zake katika mji mkuu wa Bagdad

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia matawi yake ya Bagdad katika kitongoji cha Karkha na Raswafa, inafanya semina za Quráni kwa lengo la kufundisha utamaduni wa vizito viwili katika jamii, sambamba na kuchukua tahadhari za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, washiriki wa semina hizo wanakuwa idadi ndogo kutokana na kuzingatia umbali kati ya mtu na mtu katika ukaaji.

Semina zimetolewa ndani ya misikiti na Husseiniyya na idadi kubwa ya wadau wa Quráni wenye umri tofauti wameshiriki kwenye semina hizo kutokana na ratiba zilivyo pangwa, chini ya walimu mahiri na wenye uzowefu mkubwa.

Masomo yaliyo fundishwa ni hukumu za usomaji wa Quráni, usomaji tahqiiq, tahfiidh na maarifa ya Quráni, semina za hukumu za usomaji wa Quráni zimefika (10), semina za tahqiiq (4), semina za maarifa ya Quráni (3), semina za kuhifadhi (4) na bado zinaendelea kama zilivyo pangwa.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu kila mwaka hufanya harakati mbalimbali kuhusu Quráni tukufu, lakini kutokana na mazingira ya afya ambayo taifa linapitia kwa sasa na changamoto ya kujilinda na maambukizi ya virusi vya Korona mwaka huu tumetosheka na mambo machache, ambayo tumekuwa na idadi ndogo ya washiriki katika kila jambo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: