Kumbukumbu ya kifo cha mwenye karama Qassim mtoto wa Imamu Mussa Alkaadhim (a.s)

Maoni katika picha
Leo ni kumbukumbu ya msiba mkubwa kwa wapenzi wa Ahlulbait (a.s), ni siku ya kukumbuka kifo cha mtu mwenye karama nyingi Qassim mtoto wa Imamu Mussa Alkaadhim (a.s) aliyekufa mwezi ishirini na mbili Jamadal-Uula mwaka wa (192h).

Riwaya zinasema kuwa Qassim (a.s) alihama katika mji wa babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kuelekea Iraq akiwa na msafara wa wafanya biashara, akikimbia manyanyaso waliyokuwa wakipewa pamoja na Imamu Mussa (a.s), wao ndio muendelezo wa watu wa nyumba ya Mtume na chemchem ya hekima na msingi wa rehema kwa waumini, walipewa mateso makubwa na watawala wa zama zao, jambo lililosababisha watoto wa Imamu Alkaadhim (a.s) wasambae duniani, akiwemo Imamu Ridhwa (a.s) na Qassim (a.s) aliyekua anajulikana kwa wingi wa elimu yake na uchamungu.

Qassim (a.s) alikufa baada ya kuugua maradhi makali mwaka (192h) katika ardhi ya Iraq mtaa wa Bakhamra, sehemu ambayo kaburi lake lipo hadi sasa likiwa limejengewa kubba ya dhahabu na minara mikubwa yenye karama nyingi zilizo shuhudiwa na watu wa karibu na wa mbali.

Miongoni mwa usia wake (a.s) kwa Ammi yake Shekh Alhayyi aliyeowa mmoja wa mabinti wake amasema: (Ewe Ammi.. nikifa unioshe na kunivisha sanda na unizike, ukifika wakati wa hijja nenda na binti yako pamoja na binti yangu huyu, mkimaliza kufanya ibada ya hijja nenda Madina, ukifika kwenye mlango wa Madina mshushe binti yangu katika mlango huo ataongoza njia, wewe na mke wangu nendeni nyuma yake hadi atakapo fika kwenye nyumba na kusimama mlangoni tambueni hiyo ndio nyumba yetu, ataingia katika nyumba hiyo yenye wanawake watupu na wote wajane).

Mwaka wa pili baada ya kufa kwa Qassim (a.s) Shekh Hayyu alikwenda hijja pamoja na binti wa Qassim (a.s), ikawa kama alivyo sema Qassim (a.s), binti yake aligonga mlango akafunguliwa, kisha akazungukwa na wanawake wa bani Hashim na wakamuuliza jina lake na kuhusu baba yake, akalia. Alipo toka mama yake Qassim (a.s) aliangalia kushotoni kwake na akaanza kuita: Ewe mtoto wake, ewe Qassim wake.. Wallahi huyu ni yatima wa Qassim, kisha yule binti akawaambia kuwa babu yake na mama yake wamesimama mlangoni, inasemekana kuwa mama yake Qassim alipo sikia kifo cha mwanae aliugua na hakuishi ispokua siku tatu halafu akafa.

Alikuwa (a.s) na heshima kubwa, alikuwa mtu mwema katika kizazi cha Mtume na mtoto wa Imamu mtakatifu, alipata mitihani mingi baada ya kaka yake Imamu Ridhwa (a.s), kuhusu hadhi yame yatosha riwaya iliyo pokewa na Thiqatul-Islami Shekh Kuleini katika kitabu cha Kaafi mlango wa Nassu: kutoka kwa Imamu Ali bun Mussa Ridhwa (a.s) kutoka kwa Yazidi bun Saliit kutoka kwa Imamu Alkaadhim (a.s) katika njia ya Makka kuwa Imamu alimuambia: (…Nakuambia ewe Abu Ammaarah mimi nilitoka nyumbani nikamuusia mtoto wangu Fulani na nikamshirikisha mwanangu kwa dhahiri na kumuusia peke yake kwa siri kama yangekua maamuzi yangu ningempa Uimamu mwanangu Qassim kwa jinsi ninavyo mpenda lakini maamuzi ni ya Mwenyezi Mungu mtukufu anampa amtakae).

Malalo ya Qassim (s.a) yapo umbali wa farsakh nane kutuka mji wa Hilla (makao makuu ya mkoa wa Baabil) nayo hutembelewa na watu wote, ziara yake inamambo maalum, Sayyid ibun Twausi amehimiza kumzuru kwenye kitabu chake cha Misbaahu Zaairu ameandika ziara ya Qassim bun Imamu Alkaadhim (a.s) pamoja na ziara ya Abulfadhil Abbasi bun Imamu Amirulmu-uminina na Ali Akbaru bun Imamu Hussein (a.s), kwenye mlango aliouita: (Utajo wa ziara ya waja wema na watoto wa Maimamu –a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: