Madaktari wa hospitali ya Alkafeel wamefanikiwa kupandikiza mishipa mitatu ya damu kwenye moyo wa mgonjwa mwenye umri wa miaka arubaini

Maoni katika picha
Kikosi cha madaktari wa hospitali ya rufaa Alkafeel kimefanikiwa kupandikiza mishipa mitatu ya damu kwenye moyo wa mgonjwa mwenye umri wa miaka arubaini.

Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo katika hospitali hiyo, Dokta Bashiru Ikbanaar amesema kuwa: “Hakika jopo la madaktari wetu limefanya upandikizaji wa mishipa mitatu ya damu katika moyo wa mgonjwa mwenye umri wa miaka (40) pamoja na kusafisha mishipa ya shingo ya upande wa kushoto”.

Akaongeza kuwa: “Mgonjwa alikuwa na uvimbe kwenye ubongo na maumivu ya kifua yaliyo pelekea kuziba mishipa ya damu ya kwenye ubongo”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel inajitahidi kutoa huduma bora kwa kutumia vifaa-tiba vya kisasa zaidi wakati wote, kupitia madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeiwezesha kutoa ushindani mkubwa katika hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa walio bobea katika fani mbalimbali za matibabu, pamoja na kupokea aina tofauti za wagonjwa walio katika hali tofauti za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: