Ratiba ya ubora kazini inaendelea na warsha za kujenga uwezo

Maoni katika picha
Ratiba ya ubora kazini inaendelea na warsha zinazo simamiwa na kitengo cha maendeleo endelevi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa watumishi wa kitengo cha kulinda nidhamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Hii ni moja ya ratiba muhimu inayosaidia kuongeza uwezo wa watumishi hususan katika kazi zinazofanywa ndani ya Atabatu Abbasiyya.

Tumeongea na rais wa kitengo hicho Dokta Muhammad Hassan Jaabir amesema kuwa: “Katika kukamilisha warsha inayofanywa ya ubora kazini kwa watumishi wa kitengo cha kulinda nidham, ambayo jumla ya watumishi thelathini wameshiriki”.

Akaendelea kusema: “Mawasiliano ni sekta muhimu katika ulimwengu wa kazi, husaidia kufikisha ujumbe wa mtu kwenda kwa mtu mwingine, kwa kutumia ujumbe wa maandishi au maneno au lugha ya muili au moja ya njia za mawasiliano, kisha mtu hujibu ujumbe huo kulingana na alivyo eliwa”.

Akaongeza kuwa: “Warsha ilikuwa na mada nyingi za msingi, miongoni mwa mada hizo ni: (Zana za mawasiliano, aina za mawasiliano kupitia lugha, kiwango cha kushiriki katika mawasiliano, vipaji vya mawasiliano), mwisho wa warsha mshiriki anatakiwa kujua aina za mawasiliano, zana za mawasiliano na namna ya kutumia lugha ya muili na ishara wakati wa kazi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: