Kiongozi wa idara Ustadhat Fatuma Sayyid Abbasi Mussawi amesema kuwa: “Kutokana na kujali turathi za maasumina katika Ahlulbait (a.s) tumeamua kufanya shindano hili katika kuadhimisha kuzaliwa kwa mbora wa wanawake wa duniani Fatuma Zaharaa (a.s)”.
Akaongeza kuwa: “Shindano linahusu kuandika muhtasasi wa kitabu cha (Mushahadaat mala-ul Al-Aála sherehe ya hadithul-Kisaa) cha Sayyid Muhammad Ali Halo, mihtasari hizo zitawasilishwa kwenye jopo la majaji”.
Akasema: “Mashariti ya kushiriki ni:
- 1- Umri wa mshiriki usiwe chini ya miaka 18.
- 2- Mihtasari utumwe kupitia barua pepe ya idara ya Quráni”.
Akaendelea kusema: “Shindano la wanawake tu, na mwisho wa kupokea mihtasari ni tarehe (31/1), usizidi kurasa (10) na itakayo zidi haitafanyiwa kazi”.
Akakumbusha kuwa: (Majina ya washindi yatatangazwa kupitia mtandao wa kimataifa Alkafeel baada ya kumaliza shindano, pamoja na ukurasa wa idara ya Quráni wa Facebook”.
Kwa maelezo zaidi fungua link hii