Chuo kikuu cha Al-Ameed kinaendelea kupokea wanafunzi wapya waliokubaliwa kwenye vitivo vyake

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendelea kupokea wanafunzi wapya waliokubaliwa kwenye vitivo vyake kwa mwaka wa masomo (2020 – 2021), wanaokuja kuthibitisha nafasi zao kwenye vitivo vya (udaktari – uuguzi – udaktari wa meno – famasia), hii ni hatua ya mwisho kabla ya kupelekwa majina yao katika wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu.

Tumeongea na makamo mkuu wa idara ya kanuni za chuo Dokta Alaa Mussawi kuhusu swala hilo amesema kuwa: “Kama kawaida ya chuo kikuu cha Al-Ameed kila unapo anza mwaka mpya wa masomo, hujiandaa na kukamilisha mambo yote yanayo husiana na upokeaji wa wanafunzi wapya pamoja na wazamani, kuhusu wanafunzi waliokubaliwa katika mwaka wa masomo (2020 – 2021), tumeandaa kamati maalum inayo husika na usajili wao, inakuwepo ofisini kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni kila siku ispokua Ijumaa, jukumu la kamati hiyo ni kukamilisha mchakato wa usajili kwa wanafunzi waliokubaliwa, ambapo wanafunzi hao hupokelewa katika ofisi za chuo zilizopo Karbala barabara ya (Karbala – Najafu) mkabala na nguzo namba (1238)”.

Akasisitiza kuwa: Wanafunzi wanatakiwa kuja na vielelezo vinavyo hitajika, ambavyo ni:

  1. Kitambulisho cha uraia na cheti cha kuzaliwa cha mwanafunzi (nakala ya asili na kopi /1).
  2. Kitambulisho cha uraia na cheti cha kuzaliwa cha mzazi wa mwanafunzi (nakala ya asili na kopi /1).
  3. Kitambulisho cha makazi (nakala ya asili na kopi /1).
  4. Vyeti vya kuhitimu elimu ya sekondari.
  5. Kodi ya kukubaliwa.
  6. Picha (6) za mwanafunzi.
  7. Cheti cha hali ya afya yake kutoka kwa daktari (wa kituo cha afya cha eneo analoishi mwanafunzi)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: