Maukibu za watu wa Karbala zinaomboleza kifo cha Qassim (a.s) na kutoa rambirambi zao kwenye malalo yake takatifu

Maoni katika picha
Maukibu za watu wa Karbala tukufu zinaomboleza kifo cha mtu mwenye karama nyingi Qassim mtoto wa Imamu Mussa mtoto wa Jafari Alkadhim (a.s), mbele ya malalo yake takatifu katika mji wa Qassim kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Rais wa kitengo tajwa bwana Riradh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “Hakika kuombileza msiba huu ni miongoni mwa utamaduni wa mawakibu hizi, na Ataba mbili tukufu hufadhili gari za kubeba watu, malalo imeshuhudia watu wengi wanaokuja kuomboleza msiba huu, miongoni mwa watu hao ni mawakibu za watu wa Karbala, kitengo cha maadhimisho na mawakibu husseiniyya kimefanya mchakato wote wa kukamilisha ibada ya ziara hii, wala sio mara ya kwanza kufanywa maaombolezo haya mbele ya malalo yake, kwani hufanywa kila mwaka, ni utamaduni ambao wamerithishana kizazi na kizazi”.

Akabainisha kuwa: “Mawakibu iliandaliwa mapokezi maalum yaliyo ongozwa na katibu maalum wa mazaru ya Qassim, mawakibu zimetembea kwa makundi, wakati wa matembezi yao walikua wanaimba kaswida za kuomboleza na tenzi zinazo muhusi Imamu Hussein zilizo tia huzuni katika nyoyo za waombolezaji, wakati wa kuingia katika haram yake takatifu (a.s) wakafanya majlis ya kuomboleza, ambayo waliimba qaswida na kusoma tenzi zinazo husu mateso waliyopata Ahlulbait akiwemo Qassim (a.s) na wafuasi wao”.

Akamaliza kwa kusema: “Mawakibu za watu wa Karbala hazikuishia kwenye kuomboleza peke yake, bali zimetoa huduma ya kugawa chakula kwa waombolezaji waliokuwa wanamiminika katika malalo hiyo kuhuisha kumbukumbu ya msiba huo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: