Atabatu Abbasiyya tukufu inawapa zawadi wanafunzi waliofaulu katika masomo mkoani Baabil

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na shule chini ya kitengo cha uhusiano, imetoa zawadi kwa wanafuzi waliofaulu kwenye masomo yao katika mkoa wa Baabil, wa shule za (msingi na sekondari) wa mwaka ulioisha, kama sehemu ya kuwatia moyo na kuwataka waongeze bidii katika safari ya kutafuta elimu.

Ustadh Raatibu Hassanawi kutoka idara ya uhusiano wa shule chini ya kitengo tulicho tajwa awali, ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika Atabatu Abbasiyya iko mstari wa mbele daima kusaidia makundi mbalimbali, likiwemo kundi hili la wanafunzi walioshika nafasi za kwanza kwenye mitihani, jambo ambalo tumeshuhudia leo pale wanafunzi 35 wa viwango tofauti walipo pewa zawadi kama sehemu ya kuwatia moyo waendelee kufanya juhudi zaidi katika masomo yao kwenye mazingira haya magumu ya janga la virusi vya Korona lililopelekea mambo mengi kusimama, pamoja na mazingira kuwa magumu mwaka huu lakini wamesoma kwa bidii na kushika nafasi za kwanza kwenye mitihani ya mwisho wa mwaka na kustahiki kupewa zawadi hizi”.

Akaongeza: “Tumeandaa ratiba maalum ya swala hili, ikiwa pamoja na kuwapeleka ziara katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), na kutembelea makumbusho katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya sambamba na kupata chakula ndani ya mgahawa (mudhifu) wa Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Wanafunzi walio pewa zawadi pamoja na wazazi wao wametoa shukrani za dhati kwa zawadi hizo, na wamefurahishwa sana kwa ukarimu wanaopewa na Atabatu Abbasiyya, kutokana na kufaulu kwao katika mitihani, wamesema kuwa ukarimu wanaofanyiwa ni zawadi bora zaidi kwao, wameyasema hayo walipokua ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: