Kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu mkuu wa malezi katika mkoa wa Karbala amesema yatupasa kutumia teknolojia katika ufundishaji

Maoni katika picha: Ustadh Abbasi Audah
Katika hafla ya kongamano la teknolojia kwa ajili ya Karbala linalo simamiwa na idara kuu ya malezi katika mkoa wa Karbala kwa kushirikiana na Aabatu Abbasiyya lililo anza asubuhi ya Jumamosi mwezi (24 Jamadal-Uula 1442h) sawa na tarehe (9 Januari 2021m) kulikuwa na ujumbe kutoka kwa mkuu wa idara ya malezi ya Karbala Ustadh Abbasi Audah, miongoni mwa aliyo sema ni: “Leo tunakutana na watu wanaopenda elimu na teknolojia pamoja na kuvitumia”.

Akaongeza kuwa: “Mwanaadamu anapokuwa mahala fulani anahitaji kutafakari na kuchukua maamuzi, tulipojikuta kwenye mazingira magumu kama wizara ya malezi na elimu ya juu tuliona kuwa hatuwezi kusimama kwenye jambo moja peke yake katika ufundishaji, bali ilikua ni muhimu kutumia njia mbalimbali ikiwemo teknolojia katika utoaji wa elimu”.

Akafafanua kuwa: “Nyie wote mnajua, wizara ya malezi au wizara zingine mazingira magumu tuliyo pitia kama taifa yamesababisha baadhi ya mambo kusimama yakiwemo masomo ambayo ndio msingi wa maendeleo, ikalazimika kutumia njia zingine mbadala za ufundishaji ndio tukaanza kutumia teknolojia na tukajikuta tunauwezo mkubwa kwenye sekta hiyo na hili sio kwa idara ya malezi peke yake bali hata idara zingine na wizara zinge, lazima tutumie teknolojia ili tuweze kusonga mbele”.

Akabainisha kuwa: “Tulikuta kuna walimu walio weza kufundisha masomo yao kwa njia tofauti, hatusemi kuwa tumefanikiwa mia kwa mia, lakini tumepiga hatua kubwa na tumeweka mfumo mzuri wa kuwasilisha masomo kwa wanafunzi”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunatarajia kongamano hili linufaishe taifa letu na mji wetu kipenzi, pongezi kubwa ziende kwa Atabatu Abbasiyya tukufu na kiongozi wake mkuu wa kisheria na katimu mkuu wake pamoja na kitengo cha malezi na elimu kwa kazi kubwa wanayo fanya”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: