Kituo cha utamaduni wa familia kimeanza harakati zake katika mwaka mpya kwa kufanya awamu ya nane ya program ya (kitabu changu thamani yangu)

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanza harakati zake za mwaka wa 2021m kwa awamu ya nane ya program ya (kitabu changu thamani yangu), program inayo himiza usomaji na kuchangia kuboresha utamaduni wa wanawake sambamba na kuongeza kiwango cha elimu ya wanawake, program hiyo ni kwa wanawake wa rika zote, nayo ni muendelezo wa mafanikio yaliyo patikana kwenye awamu zilizo tangulia, idara ya kituo imeamua kuendeleza program hii.

Mkuu wa kituo bibi Asmahani Ibrahim amesema kuwa: “Program hii imepata muitikio mkubwa, kila awamu inakua na mafanikio makubwa tofauti na awamu iliyo tangulia, ndio sababu iliyopelekea kuendelea na program hadi kufikia awamu hii ambayo kituo kimefungulia mwaka 2021m”.

Akaongeza kuwa: “Katika awamu hii tutauliza maswali yanayo jikita katika kutambua uwelewa wa washiriki na uwezo wa kufanyia kazi mambo hayo katika maisha yao ya kila siku, muda wa kushiriki kwenye shindano hili ni siku (15) za kusoma na kufanya mtihani, kutakuwa na zawadi za washindi watatu kwa kwanza watakao patikana baada ya kupigiwa kura majibu sahihi”.

Akabainisha kuwa: “Washindi watapewa taarifa baada ya kumaliza shindano na kuchambua majibu sahihi”.

Kumbuka kuwa program hii inalenga kujenga utamaduni wa kujisomea na kutumia muda kwa mambo yenye manufaa na kujenga kujiamini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: