Hivi karibuni kituoa cha turathi za Hilla chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetoa jarida la kumi na saba la (Raddu-Shamsi), nalo ni jarida linalo andika tamaduni tofauti sambamba na turathi za mji wa Hilla.
Jarida linajumla ya kurasa (106) limejaa Makala za turathi na historia za mji wa Hilla.
Kiongozi wa kituoa cha turathi za Hilla Shekh Swadiq Khawilidi amesema kuwa: “Kwa baraka za Mwenyezi Mungu na utukufu wa mbeba bendera tumeandika jarida la (Raddu-Shamsi) tolea la kumi na saba, linalo endana na matoleo yaliyo tangulia”.
Akaongeza kuwa: “Toleo hili linamakala nyingi katika kurasa mia moja na sita zilizo beba maudhui tofauti, miongoni mwa maudhui hizo ni familia za Hilla, mlango wa malalo na mazaru, pamoja na maelezo marefu kuhusu Ashura, na mhanga wa Imamu Hussein na jinsi athari yake ilivyo endelea pamoja na baraka zake hadi leo”.
Akaendelea kusema: “Tumeandika kuhusu wanachuoni wa Hilla na wanachuoni wakubwa wa kiislamu, waandishi wakubwa wameshiriki kuandika jarida hili”.
Kumbuka kuwa jarida la (Raddu-Shamsi) ni moja ya machapisho yanayotolewa na kituo hiki, nalo limejikita katika kuandika turathi za Ahlulbait (a.s) na turathi za mji wa Hilla na historia yake.