Kumaliza hatua ya kwanza ya uwekaji wa marumaru katika sehemu ya jengo la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Mafundi wanaofanya kazi ya kuweka marumaru za ukutani na sehemu ya chini katika jengo la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), upande wa kulia kwa ndani hadi kwenye haram takatifu katika hatua ya kwanza, inayo husisha sehemu ya ukuta wa haram na makutano ya haram takatifu.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh amesema kuwa: “Mradi huu unakamilisha kazi zilizo tangulia, ambazo ni kuondoa tabaka la sakafu ya zamani na kusawazisha ardhi pamoja na kuweka zege, na hivi sasa tumeweka marumaru ukutani na chini katika eneo la nguzo na kuchukuliwa kama msingi wa ujenzi katika eneo hilo la haram tukufu”.

Akabainisha kuwa: “Marumaru tulizo tumia ni aina ya (Malt-Oksi), ambayo ndio aina iliyowekwa ndani ya haram tukufu, pamoja na sifa zingine zinazo zifanya marumaru hizo kuwa bora zaidi na kufanya eneo hilo kuwa na muonekano mzuri pamoja na maeneo mengine”.

Kumbuka kuwa mradi wa kuweka marumaru ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ni sehemu ya kukamilisha miradi iliyofanywa hapo awali, kazi hii imefanywa kutokana na kuharibika kwa marumaru za zamani kwa sababu ya ukongwe wake kwani zilikua na zaidi ya miaka (50), ndio Atabatu Abbasiyya ikaamua kufanya mradi huu kwa lengo la kupendezesha muonekano wa sehemu hiyo, na kuifanya kuwa na muonekano mzuri unaotia furaha katika nafsi za mazuwaru watukufu, kazi ya kuweka marumaru sehemu ya pambo la dhahabu ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), imefanyika sambamba na kuweka dhahabu kwenye ukuta unaobeba pambo hilo (sega).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: