Zaidi ya kesi 1500 kwa mwezi: Huduma za matibabu ya meno bure hutolewa katika chuo kikuu cha Alkafeel

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kitengo cha tiba ya meno kinatoa huduma bure kwa zaidi ya wagonjwa 1500 ndani ya mwezi, kwa makundi ya watu tofauti.

Hayo yamesemwa na mkuu wa kitengo hicho Dokta Muayyad Fadhili Zawin, akaongeza kuwa: “Hiki ni miongoni mwa vituo muhimu katika mkoa mtukufu wa Najafu, kila siku tunapokea zaidi ya wagonjwa (50) na idadi inazidi kuongezeka, tunatibu maradhi ya meno ya aina tofauti, tunasafisha, kuziba, kuweka meno bandia, kuweka mizizi ya meno (fizi) pamoja na mambo mengine (tatizo la kupandana meno na fizi – kurepea meno yote – urekebishaji wa meno ya watoto – kusafisha meno na kuimarisha fizi), kuna hali ambazo zinahitaji zaidi ya kikao kimoja, tunapokea wagonjwa wa umri na jinsia tofauti”.

Akabainisha kuwa: “Vifaa tiba tunavyo tumia ni vya kisasa na vyenye ubora mkubwa, aidha vimethibitishwa na kuidhinishwa na wizara ya afya ya Iraq, wagonjwa hutibiwa kwa hatua mbili kisha hatua ya nne na tano huwa chini ya daktari bingwa wa meno”.

Akamaliza kwa kusema: “Hakika kitengo cha meno kimekuwa na wagonjwa wengi, kutokana na weledi wa madaktari wake ambao ufanisi wao unaonekana wazi katika utoaji wa huduma, wamejenga uaminifu mkubwa katika aina zoto za tiba ya meno kutoka kwa wagonjwa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: