Hatua kubwa imepigwa katika utengenezaji wa umbo la mbao la dirisha la bibi Zainabu (a.s) na kazi inaendelea katika sehemu zake za kuwekwa madini

Maoni katika picha
Utengenezaji wa umbo la mbao katika dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s) linalo tengenezwa ndani ya kitengo cha utengenezaji wa madirisha ya kwenye makaburi matakatifu na milango mitukufu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu umepiga hatua kubwa, juu ya kiwango kilicho kadiriwa, na kazi ya kutengeneza sehemu zitakazo wekwa madini inaendelea, kila kipande cha madini kitakacho kamilika kitawekwa kwenye dirisha moja kwa moja, kama mchoro unavyo onyesha na kupitishwa na kamati inayo simamia mradi huu.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo hiko Sayyid Naadhim Ghurabi, akaongeza kuwa: “Kazi ya kutengeneza dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s) iliwekewa mpango kazi maalum unao onyesha utendaji wa kazi zote pamoja na ufafanuzi wa utendaji wake, miongoni mwa kazi ambazo zimepiga hatua kubwa katika utendaji wake ni utengenezwaji wa umbo la mbao, ambayo ni kazi muhimu sana katika mradi huu, kwa sababu ndio msingi wa kuelekea katika sehemu zingine”.

Akaongeza kuwa: “Mafundi selemala wameandaa kila kitu kinacho hitajika katika mradi huu, na wametengeneza kila kitu kwa utaalamu na umaridadi mkubwa kwa kutumia vifaa bora na imara zaidi, wamechagua mbao bora za (Burumi) wamezichonga kwa umaridadi na kuzingatia uzito zitakao beba”.

Akaendelea kusema: “Umbo la mbao katika dirisha hilo ni la mstatiri na linanguzo nne kubwa na kumi ndogo zinazo zunguka dirisha, halafu kuna leli kubwa za mbao nne kwa chini zinazo beba nguzo kuu, na zitawekwa madini ya silva safi yenye ujazo wa (ml 5) kwa ajili ya kuongeza uimara na kudumu kwa muda mrefu, pia kuna leli zingine kuu nne za juu zitakazo fungwa nguzo kuu kwa juu, vilevile sehemu ya juu inafito zitakazo wekwa mapambo na maandishi pamoja na paa”.

Amesisitiza kuwa: “Kazi ya kutengeneza sehemu za madini inaendelea vizuri, tayali sehemu zote za vipande vya madini zimesha anza kutengenezwa, sasa hivi wanaendelea na kutengeneza sehemu za mapambo ya dirisha na vitako vya nguzo vitakavyo beba dirisha, sambamba na kutengeneza sehemu zinazo unganisha baina ya madirisha madogomadogo, kazi hii inahitaji umakini wa hali ya juu kwani inafanywa kwa mikono, na kazi ya kutengeneza vifuniko vitakavyo wekwa kwenye dirisha bado inaendelea”.

Kumbuka kuwa mafundi wa Atabatu Abbasiyya wanaotengeneza madirisha ya kuweka kwenye makaburi na mazaru matukufu, wanaujuzi na uzowefu mkubwa katika kazi hiyo, walionyesha kwa vitendo uwezo wao pale walipo tengeneza dirisha la kaburi la Abuladhil Abbasi (a.s) kisha wakatengeneza dirisha la maqaam ya Swafi-Swafa, dirisha la Qassim (a.s), milango ya malalo ya Sayyid Muhammad –Sabúdujail), dirisha la Shekh Mufidi na Shekh Tusi, sehemu ya juu ya dirisha la Maimamu wawili Aljawadaini (a.s) na kazi zingine nyingi, pamoja na sehemu ya mbele ya dirisha la Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) na sehemu ya juu ya dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s), na kazi inayo endelea hivi sasa ya dirisha la Maqaam ya mkono na dirisha la Maqaam upande wa wanawake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: