Kituo cha turathi za Basra kinawalenga vijana kwenye maonyesho maalum

Maoni katika picha
Katika harakati zake kwa kushirikiana na kitengo cha harakati na michezo ya shuleni katika idara kuu ya mkoa wa Basra, kitengo cha turathi za Basra chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanya maonyesho ya vitabu vya turathi ndani ya ukumbi wa michezo katika wilaya ya Shatul-Arabu/ kitongoji cha Kabasi.

Maonyesho hayo yamejaa vitabu mbalimbali vilivyo andikwa na kituo hicho, pamoja na mabango ya picha za turathi tofauti zilizopo katika mji huu, hali kadhalika kuna nakala-kale adumu zinazo eleza historia ya mji huu, zilizo andikwa na wanachuoni wa zamani katika miongo tofauti.

Tambua kuwa maonyesho yanalenga wanafunzi wa shule za sekondari, kwa ajili ya kuwafundisha turathi za mji wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: