Miongoni mwa machapisho ya kituo cha turathi za Karbala ni kitabu cha (Nyaraka za Ataba takatifu za Iraq)

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeandika sehemu zote za wakfu Shia na mazaru tukufu za kishia zilizopo Iraq, sambamba na kuandika majina ya Ataba takatifu tangu mwaka 2003 hadi mwaka 2016 na kutengeneza jeduwali linalo onyesha kila sehemu kupitia jina la (Nyaraka za Ataba takatifu za Iraq), pamoja na kuchapisha jarida maalum kuhusu Ataba hizo, kila kitu kimeandaliwa kwa kufuata mfumo wa kielimu unaokubalika kulingana na ukubwa wa jambo husika.

Tumeongea na mkuu wa kituo Dokta Ihsaan Ghuraifi kuhusu mradi huu, amesema kuwa: “Kitabu kimeandikwa katika mfumo wa milango chini ya utaratibu maarufu duniani wa nyaraka, limeandikwa jarida la kwanza kisha jarida la pili na la tatu kwa kila Ataba au Mazaru na kwa ufafanuzi kama ifuatavyo: (Atabatu Alawiyya – Atabatu Husseiniyya – Atabatu Abbasiyya – Atabatu Kadhimiyya – Masjidi Kufa na sehemu zake – Diwani wakfu Shia/ ofisi kuu – Mazaru tukufu zingine)”.

Kumbuka kuwa kituo cha turathi za Karbala kinaendelea kuandika vitabu na majarida, pamoja na mtiririko wa turathi za mji wa Karbala baada ya kufanya uhakiki na utafiti, ili kuchangia katika maktaba za kiarabu na kiislamu kwa kuingiza machapisho hayo, na kuonyesha mchango wa mji wa Karbala katika sekta zote za elimu na maarifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: