Kiwanda cha Al-Atwaa kimeongeza uzalishaji na uongozi wake umesema kuwa bidhaa zao ni bora

Maoni katika picha
Kiwanda cha Al-Atwaa kinacho tengeneza bidhaa za ujenzi (kokoto na zinginezo) kimesema kuwa kimeongeza uzalishaji wake unaokidhi vigezo vya kitaifa na kimataifa, hivyo bidhaa zake zinatumiwa na mashirika pamoja na watu binafsi, kwa kiwango kinachosaidia upatikanaji wa bidhaa hizo katika soko na kuondoa upungufu uliokuwepo.

Hayo yamesemwa na Mhandisi Alaa Jaburi mkuu wa kiwanda hicho, akaongeza kuwa: “Siku baada ya siku viwanda vilivyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu vinathibitisha ubora wake, jambo ambalo limevifanya kuwa kimbilio la watumiaji wa bidhaaa zake, miongoni mwa viwanda hivyo ni hiki cha kutengeneza bidhaa za ujenzi, hivyo kimelazimika kuongeza uzalishaji wake”.

Akabainisha kuwa: “Kiwanda kina sehemu nne, sehemu ya kuzalisha kokoto, zinatengenezwa kokoto za aina mbili na zenye ukubwa tofauti, na sehemu ya kuzalisha mchanga wa aina tofauti, na sehemu mbili za kuzalisha changarawe za aina tofauti”.

Akasisitiza kuwa: “Bidhaa zote zinazo tengenezwa hupimwa na kuthibitishwa ubora wake katika maabara ya kitengo cha miradi ya kihandisi au maabara zingine, mara zote hutoa majibu mazuri na hukidhi viwango vinavyo takiwa, hii ndio sababu kubwa ya kuwa kimbilio la mashirika ya ujenzi pamoja na watu binafsi”.

Kumbuka kuwa kiwanda cha Al-Atwaa kilianzishwa kwa ajili ya miradi ya ujenzi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kutokana na dhana ya kujitegemea na mambo yafuatayo yamefanikishwa:

  • - Kutoa ajira.
  • - Kupata vifaa vyenye ubora mkubwa.
  • - Kutumia malighafi za kawaida na kuzielekeza kwenye matumizi sahihi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: