Mchango wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa walioitikia wito wa fatwa katika mwaka 2020m ni zaidi ya milioni 120 dinari na bado inaendelea

Maoni katika picha
Kamati ya misaada na maelekezo chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu imetaja kiwango ilichotoa kusaidia watu walioitikia wito wa fatwa tukufu ya kujilinda ndani ya mwaka 2020m kuwa zaidi ya milioni 120 dinari walizopewa vikosi tofauti vya askari, pamoja na kuwepo kwa changamoto ya janga la virusi vya Korona na kusimama shughuli za kamati hiyo kwa zaidi ya miezi mitatu, lakini iliendelea na mwenendo wake wa kusaidia askari watukufu kwa kuwapa chakula, matandiko, shuka na mambo mengine waliyokuwa wanahitaji kulingana na uwezo wetu.

Haya yamesemwa na kiongozi wa idara hiyo Shekh Haidari Aaridhwi, akaongeza kuwa: “Tangu ilipotolewa fatwa takatifu na Marjaa Dini mkuu Atabatu Abbasiyya imekuwa na mchango mkubwa kwenye uwanja wa vita, kupitia kamati ya misaada na maelekezo iliyo undwa baada ya kutolewa fatwa hiyo takatifu, na kuchukua jukumu la kusaidia askari kwa kuwapa mahitaji ya lazima”.

Akabainisha kuwa: “Misaada imekuwa ikitolewa kwa wapiganaji wa Hashdu-Shaábi na askari wa serikali, tumetoa zaidi ya dinari milioni 120, kama mazingira yangekuwa rafiki tungetoa zaidi ya pesa hizo, lakini kutokana na hali ya mazingira ya afya na marufuku ya kutembea iliyo wekwa imesababisha kutoa misaada chini ya kiwango, lakini tuliamua kubadilisha muelekeo na kusaidia familia za watu wenye kipato kidogo na mafakiri walio athiriwa na marufuku ya kutembea, tutatangaza kiwango tulicho saidia upande huo chini ya opresheni isemayo (Marjaiyyatu-Takaaful)”.

Akamaliza kwa kusema: “Misaada inatolewa na kamati za mikoani zilizo chini yetu zenye jukumu la kuwasiliana na vikosi vya askari, pamoja na kwenda kukutana nao na kuangalia hali zao, sambamba na kuwapa usia na nasaha pamoja na mambo mengine”.

Kumbuka kuwa kamati ya misaada na maelekezo iliyo anzishwa baada ya kutolewa fatwa tukufu ya kulinda taifa la Iraq na maeneo matakatifu na kuwa miongoni mwa kamati za kwanza kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu wa kusaidia wanajeshi na wapiganaji wa kujitolea pamoja na majeruhi wao, na ikatoa mchango mkubwa katika vita hadi ukapatikana ushindi dhidi ya magaidi wa Daesh na kufanikiwa kukomboa ardhi yote ya Iraq, misaada yao ilikuwa ya aina tofauti, kuanzia kusaidia wapiganaji kwenye uwanja wa vita, familia zao mashahidi na majeruhi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: