Namna gani mashamba ya Atabatu Abbasiyya yamechangia kusaidia uzalishaji wa ndani na kuaminiwa na wananchi

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imeipa kipaumbele sekta ya kilimo, kupitia miradi tofauti ya sekta hiyo, inayo saidia kujitosheleza katika upatikanaji wa chakula kupitia aina tofauti za mazao ya kilimo yanayo tumiwa kwa chakula na wananchi, miongoni mwa miradi hiyo ni shamba la Khairaat Abulfadhil Abbasi (a.s) lililo chini ya shirika la uchumi Alkafeel, ambalo linatumia vifaa vya kisasa katika ulimaji wake, vinavyo tumiwa na nchi zilizo endelea ulimwenguni, kuanzia mbegu -green house-, mfumo wa umwagiliaji, dawa za kupambana na maradhi ya mimea na mambo mengine, mambo yanayo saidia kupata mavuno makubwa na mimea yenye ubora mkubwa.

Haya yamesemwa na Mhandisi Ali Mazáli Laaidh rais wa kitengo cha kilimo na ufugaji, akaongeza kuwa: “Mashamba haya yameandaliwa kwa ajili ya kilimo cha kijani, kama vile nyanya, bilinganya, pilipili kali na baridi pamoja na matango, sambamba na mazao hayo huwa tunapanda mazao maarufu katika jamii, kama vile nyanya za Karziyya, Lahanah na karnabiit”.

Akabainisha kuwa: “Ulimaji wa mashamba hayo unamitazamo mingi, mazao tuliyo taja yanatumiwa kwa wingi na wananchi kila siku, na upande mwingine tunazalisha mazao yenye ubora mkubwa na tunauza kwa bei rahisi anayoweza kuimudu kila raia wa Iraq, hivyo mazao yetu ni mkombozi wa raia mwenye kipato kidogo”.

Kuhusu malengo ya miradi hiyo amesema kuwa: “Mradi unamalengo mengi miongoni mwake ni:

  • - Kutumia sehemu kubwa ya ardhi.
  • - Kuchangia uzalishaji wa ndani na kutimiza dhana ya kujitegemea, mashamba yetu yanachangia zaidi ya asilimia %20 ya mahitaji ya chakula.
  • - Kutoa ajira kwa watu wengi zaidi kupitia sekta hii muhimu, ambayo imepata muitikio mkubwa katika siku za karibuni kutokana na changamoto zilizo jitokeza kwenye miradi yao.
  • - Kushawishi wakulima watumie mbinu za kisasa katika ulimaji wao.
  • - Shamba darasa maalum kwa ajili ya mafunzo ya kilimo na utafiti.
  • - Kuzalisha mazao yenye ubora mkubwa na kuuzwa kwa bei rahisi, kwani tunatumia mbolea ya kienyeji isiyokuwa na kemikali”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imechangia kwa kiwango kikubwa kuingiza mazao bora ya kilimo katika soko la ndani, kwani inatumia mbolea ya kienyeji isiyokuwa na kemekali zenye madhara kwa afya ya mwanaadamu, sambamba na upatikanaji wa mazao hayo kwa bei ndogo anayo weza kuimudu hata mtu mwenye kipato kidogo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: