Kuanza usajili wa semina ya Faidhu-Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanza kusajili washiriki wa semina ya Faidhu-Zaharaa (a.s) itakayo fanyika kwa njia ya mtandao kwa wanawake, kama sehemu ya kukumbuka kifo chake (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa kituo hicho bibi Asmahani Ibrahim amesema: “Itakua semina elekezi yenye mada mbalimbali za kimalezi, kutoka katika historia takatifu ya bibi Zaharaa (a.s), yeye ndio mfano bora katika masomo ya kimaadili, hii ni sehemu ya tatu, sehemu ya kwanza na ya pili zilikuwa na muitikio mkubwa”.

Semina hii itadumu kwa muda wa siku tatu kwenye jukwaa la telegram kupitia link ifuatayo https://t.me/faydalzahraa2 kuanzia siku ya Jumapili (3 Jamadal-Aakhar), chini ya ukufunzi wa wahadhiri mahiri, kutakuwa na nafasi ya majadiliano na maswali kutoka kwa washiriki”.

Akafafanua kuwa: “Semina itakuwa na mada kuu zifuatazo:

  • - Mfumo wa bibi Fatuma Zaharaa (a.s) katika malezi ya watoto.
  • - Majukumu ya nyumbani na ulezi wa familia kutoka bibi Zaharaa (a.s).
  • - Misingi mikuu ya maisha ya ndoa ya bibi Zaharaa (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: