Ugeni kutoka chuo kikuu cha Bagdad umetembelea Atabatu Abbasiyya na kukutana na kiongozi wake mkuu wa kisheria

Maoni katika picha
Adhuhuri ya Ijumaa ya leo ugeni kutoka kitivo cha uhandisi – Alkhawarazami/ chuo kikuu cha Bagdad umetembelea Atabatu Abbasiyya tukufu, baada ya kufanya ibada ya ziara, ugeni huo umekutana na Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Ataba tukufu Sayyid Ahmadi Swafi.

Ziara hii ni sehemu ya ziara nyingi zinazo fanywa na vyuo vikuu vya Iraq katika Atabatu Abbasiyya tukufu, zinazo lenga kuimarisha uhusiano na Ataba tukufu, kwa ajili ya kubadilishana uzowefu na kushirikiana katika mambo yenye faida kwa pande zote mbili.

Tumeongea na rais wa ugeni huo ambaye ni rais wa kitivo cha uhandisi Dokta Maahir Yahya Salum amesema kuwa: “Leo tumetembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na kukutana na kiongozi wake mkuu wa kisheria, kikao kimekuwa na faida kubwa, tumeongea mambo mengi yanayo husu elimu ya vyuo vya Iraq na mbinu za kuiboresha, sambamba na kujadili changamoto mbalimbali zinazo ikumba sekta ya elimu”.

Akaongeza kuwa: “Vyuo vya Atabatu Abbasiyya tukufu vinamaendeleo makubwa, tunatarajia kunufaika na uzowefu wake katika ufundishaji na utumiaji wa teknolojia za kisasa, Insha-Allah tutatembelea chuo kikuu cha Alkafeel na kuangalia ufundishaji wao pamoja na vifaa wanavyo tumia, darasani na ofisini”.

Akaendelea kusema: “Tunatarajia kuwa na ushirikiano kati yetu na vyuo vya Atabatu Abbasiyya kwa faida ya sekta ya elimu hapa nchini”.

Mkuu wa chuo kikuu cha Alkafeel Dokta Nuris Dahani akasema kuwa: “Tumeongea mambo mengi muhimu ikiwa ni pamoja na ushirikiano kati ya kitivo cha uhandisi katika chuo kikuu cha Bagdad pamoja na vyuo vikuu vya Atabatu Abbasiyya tukufu, Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya amewaalika wageni hao kutembelea chuo kikuu cha Alkafeel kuangalia mfumo wa majengo yake na maabara pamoja na ratiba za ufundishaji kwa njia za mitandao zinazo tumika kwa sasa, pamoja na kuangalia uwezekano wa chuo kikuu cha Khawarazami kutumia program ya mtandao wa ufundishaji katika vyuo vikuu tulio tumia mwaka jana”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: