Waziri wa kilimo amepongeza miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya kilimo

Maoni katika picha
Waziri wa kilimo Mhandisi Muhammad Khafaji amepongeza miradi ya kilimo inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, na akasifu kazi kubwa inayofanywa ya kuendeleza sekta hiyo, na kurudisha utambulisho wa kilimo katika taifa.

Waziri ameyasema hayo alipotembelea miradi ya kilimo akiwa pamoja na ujumbe aliofuatana nao jioni ya Ijumaa (1 Jamadal-Aakhar 1442h) sawa na (15 Januari 2021m) katika mradi wa Firdausi (moja ya miradi muhimu ya kilimo inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu), katika ziara hiyo alifuatana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Muhammad Ashiqar na msimamizi wa sekta ya kilimo.

Mheshimiwa waziri amesikiliza maelezo kutoka kwa wasimamizi wa mradi huo, kuhusu mazao wanayolima na teknolojia ya kisasa wanayo tumia pamoja na mafanikio yanayo patikana. Pembezoni mwa ziara hiyo alitembelea jengo la shule la kwanza na la tatu, akafurahishwa sana na mambo aliyo yaona katika majengo hayo.

Mwishoni mwa ziara hiyo akafanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na akawashukuru watumishi wa Atabatu Abbasiyya na kupongeza huduma nzuri wanazo toa kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: