Shule za Dini Alkafeel za wanawake zinaomboleza kifo cha Swidiqah Twahirah (a.s)

Maoni katika picha
Asubuhi ya Jumamosi mwezi pili Jamadal-Aakhar 1442h, sawa na tarehe (16 Januari 2021m), idara ya shule za Dini Alkafeel tawi la wanawake chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya maonyesho ya igizo la tukio la kifo cha bibi Fatuma Zaharaa (a.s), ndani ya ukumbi wa jengo la Shekh Kuleini (r.a) na kuhudhuriwa na kundi kubwa la walimu wa kike na wanafunzi wao.

Kiongozi wa idara hiyo bibi Bushra Kinani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Shule za Dini za Alkafeel zipo kwenye mikoa mingi ya Iraq, katika kila shule tumeunda maukibu au kamati ya Husseiniyya yenye jukumu la kuandaa shughuli mbalimbali, pamoja na kufanya maigizo yanayo husu matukio ya kihistoria yenye athari kwa watu wa rika zote, leo tumeshuhudia igizo lililo andaliwa na maukibu ya Ummul-Banina (a.s) iliyo chini ya shule ya Albatuli (a.s) katika mkoa wa Muthanna”.

Akabainisha kuwa: “Jumla ya watu (30) wameshiriki katika maonyesho ya igizo hilo lililodumu kwa muda wa saa mbili, sambamba na kufuata kanuni zote za kiafya, kama vile kuvaa barakoa na kutumia vitakasa mikono”.

Kumbuka kuwa idara ya shule za Dini Alkafeel tawi la wanawake, imezowea kuadhimisha matukio ya maimamu wa Ahlulbait (a.s) katika matawi yake yote, kwa kufanya shughuli mbalimbali yakiwemo maigizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: