Idara ya kufuatilia adabu za ziara inatoa mafunzo kwa watumishi (60) wa kujitolea

Maoni katika picha
Idara ya adabu za ziara katika ofisi ya tablighi chini ya kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, inatoa mafunzo kwa watumishi (60) wa kujitolea ili kuwafanya waweze kutoa huduma zao kwa weledi, kiongozi wa idara hiyo Sayyid Hassan Aáraji amesema kuwa: “Watu hao wamejitolea kusaidia watumishi wa kitengo hicho katika ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, kama vile ziara ya Arubaini, siku za Ashura, ziara ya Shaábaniyya, siku ya Arafa, siku za Ijumaa na zinginezo, mafunzo haya yanalenga kuboresha utendaji wao”.

Akaongeza kuwa: “Watumishi hao (60) wa kujitolea tumewagawa makundi mawili, kila kundi linawatu (30) kwa ajili ya kuweza kuwafikia kwa urahisi na kuwafanya waelewe vizuri masomo, kitengo cha maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya kimewaandalia semina maalum itakayo dumu siku tatu, miongoni mwa mambo watakayo fundishwa ni:

Kwanza: mbinu za kuamiliana na mazuwaru.

Pili: mbinu za kuamiliana na athari za mawasiliano.

Tatu: kutatua changamoto na maoni ya kifikra.

Nne: mbinu za utendaji bora wa majukumu”.

Akaongeza kuwa: “Watu hawa walikua wanafanya kazi kwa kujitolea muda mrefu, wamekua msaada mkubwa kwa utendaji wa vitengo vingi vya Ataba, ni wajibu wetu kuwapa mafunzo rasmi watu hawa, kwani wanawakilisha Ataba tukufu katika kutekeleza majukumu yake, na wanahudumia mazuwaru moja kwa moja”.

Akabainisha kuwa: “Watu hawa watafanya kazi siku tatu kwa wiki (Alkhamisi, Ijumaa na Jumamosi) kwa zamu, watakua bega kwa bega na watumishi wa idara wanayo saidia”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: