Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba ya kuomboleza kifo cha Zaharaa (a.s).

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba ya kuomboleza kifo cha mbora wa wanawake wa ulimwenguni Swidiiqatu-Kubra Fatuma Zaharaa (a.s) –kwa mujibu wa riwaya ya tatu-.

Ratiba inavipengele vingi, kuna mihadhara ya kidini, majlizi maalum za kuomboleza, pamoja na kujiandaa kupokea mawakibu za waombolezaji kutoka ndani na nje ya mji wa Karbala, zinazo kuja kumpa pole Imamu Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), ratiba hii inakamilisha ratiba zilizo andaliwa na kutekelezwa kwenye tukio kama hili kwa mujibu wa riwaya ya pili.

Ratiba itakua na mambo yafuatayo:

  • - Kufanya majlisi za kuomboleza asubuhi na jioni kwa muda wa siku tatu mfululizo, ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) chini ya usimamizi wa idara ya wahadhiri wa Husseiniyya.
  • - Kutoa mhadhara wa kuomboleza kupitia kitengo cha Dini siku ya kumbukumbu ya kifo chake.
  • - Kuandaa majlisi za kuomboleza zitakazo hudhuriwa na wanawake ndani ya sardabu ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
  • - Kutakuwa na mihadhara ya wanawake ndani ya jengo la Shekh Kuleini, itakayo ratibiwa na idara ya shule za Alkafeel za Dini.
  • - Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya tukufu kitaandaa shindano na mihadhara kwa njia ya mtandao.
  • - Kuandaa majlisi ya kuomboleza ya masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
  • - Kuandaa ratiba ya kupokea mawakibu za waombolezaji kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala kupitia kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili takatifu.
  • - Kufungua usajili wa ziara ya bibi Zaharaa (a.s) kupitia dirisha la ziara kwaniaba katika mtandao wa kimataifa Alkafeel.
  • - Kuweka mapambo meusi katika haram.
  • - Kufanya program mbalimbali za kuomboleza kwa kushirikiana na kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu, kama mihadhara na maigizo.
  • - Kitengo cha mgahawa (mudhifu) kitagawa mamia ya sahani za chakula kwa mazuwaru na waombolezaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: