Kuondoka kwa uwa la moyo muombezi wa umma

Maoni katika picha
Siku ya leo mwezi (3 Jamadal-Aakhar) ni kumbukumbu ya kifo cha mbora wa wanawake wa duniani na pande la damu ya Mtume (s.a.w.w) na mke wa kiongozi wa waumini (a.s) mama wa maimamu watakasifu (a.s) Fatuma binti Rasuulu-Llahi –a.s- kwa mujibu wa riwaya ya tatu.

Riwaya zinaonyesha kuwa bibi Zaharaa (a.s) alipokaribia kufa alimuusia kiongozi wa waumini (a.s) mambo mengi, miongoni mwa mambo aliyo husia ni: (… nakuusia utakapofika wakati wa kuongoka duniani, unioshe na wala usinifunue, mimi ni msafi (twahiri) na uniweke marashi aliyo niwekea baba yangu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), uniswalie pamoja na watu wa karibu zaidi miongoni mwa watu wa nyumbani kwangu, unizike usiku wala sio mchana baada ya kutulia na macho ya watu kulala, unizike kwa siri sio dhahiri, ufiche sehemu ya kaburi langu, wala jeneza langu lisishuhudiwe na yeyote miongoni mwa walio nidhulumu).

Siku ya kuondoka kwake duniani (a.s) aliwachukua watoto wake Hassan na Hussein (a.s) akawaogesha na kuwapikia chakula cha siku hiyo, kisha akawaambia waende kutembelea kaburi la babu yao, huku akiwaangalia jicho la kuwaaga na moyo wake unamuuma, akamwita Asmaa binti Umais aliyekua muuguzi wake, akasema (a.s): “Niogeshe” Asmaa akachukua maji na kumuogesha (a.s), kisha (a.s) akamuambia “niletee mguo mpya” Asmaa akampa nguo mpya. Halafu akasema “weka tandiko langu katikati ya nyumba” Asmaa moyo wake ukashtuka, akatambua kuwa kifo kimekaribia kwa Zaharaa (a.s), akamfanyia kila alicho taka, bibi Zaharaa (a.s) akalala juu ya tandiko lake na akaelekea kibla, akaanza kusoma Quráni tukufu hadi roho yake ilipoondoka duniani.

Zilipo sambaa habari za kifo chake (a.s) watu wa Madina wakajaa katika mlango wa Imamu Ali (a.s) wakisubiri kushindikiza jeneza lake (a.s), Imamu Ali (a.s) akamuambia Salmaan awaambie watu kuwa mazishi yake hayatofanyika jioni ya siku hiyo, watu wakaondoka. Ulipoingia usiku Imamu Ali (a.s) akamuosha akiwa na bibi Asmaa.

Kabla ya kumuandaa Imamu (a.s) alimwita Hassan na Hussein waje kumuaga mama yao na kumuangalia jicho la mwisho, baada ya kumaliza Imamu (a.s) alimfunika shuka (sanda) kisha akamswalia, halafu akawaambia bani Hashim na wafuasi wake wa karibu wabebe jeneza lake na kumpeleka katika nyumba yake ya milele wala wasimuambie yeyote kuhusu jambo hilo, ispikua watu hao wachache katika wafuasi wake na watu wa nyumbani kwake.

Imamu Ali (a.s) alisimamia mazishi yake, baada ya kumaliza alisimama (a.s) mbele ya kaburi na akasema: “Amani iwe juu yako ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu kutoka kwangu na kwa binti yako aliyelala jirani yako, amekutana na wewe haraka, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu subira yangu imekua ndogo, ngozi yangu imesinyaa kutokana na msiba huu, hakika ni majonzi makubwa na msiba uumizao, nimemuweka kaburini kwa mikono yangu, huku majonzi yakiwa yamenijaa kifuani mwangu”.

Amani iwe juu yake siku aliyo zaliwa na siku aliyo kufa kishahidi akiwa ni mdhulumiwa na siku atakayo fufuliwa akiwa mwenye kuridhia na kuridhiwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: