Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanya majlisi ya kukumbuka kifo cha bibi Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu, nayo ni miongoni mwa ratiba ya uombolezaji iliyoandaliwa na Atabatu Abbasiyya kufuatia tukio hili chungu, ambalo liliutikisa umma wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) katika siku kama ya leo (mwezi tatu Jamadal-Aakhar mwaka 11 hijiriyya).
Majlisi imefanywa ndani ya ukumbi wa utawala katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefunguliwa kwa Quráni iliyosomwa na Muslim Shabaki, ukafuata mhadhara uliotolewa na Shekh Muhammad Alkuraitwi kutoka kitengo cha Dini, amezungumza mambo mengi na hatua alizo pitia Fatuma Zaharaa (a.s), sambamba na kueleza baadhi ya utukufu wake uliotajwa ndani ya Quráni na nafasi yake kwa Maimamu na Mitume (a.s), na utukufu aliopewa wa ridhaa ya Fatuma ni ridhaa ya Mwenyezi Mungu na kuchukia kwa Fatuma ni kuchukia kwa Mwenyezi Mungu, akaongea pia kuhusu umaasumu wa bibi Zaharaa (a.s) kwa dalili za kiakili na kinakili, pamoja na kueleza subira ya kiongozi wa waumini (a.s) kutokana na yale yaliyo mkuta bibi Zaharaa (a.s).
Akamaliza mhadhara wa majlisi kwa kusoma tenzi kuhusu msiba huu adhimu na wenye kutia majonzi makubwa katika nyoyo za waumini, tenzi hizo ziliamsha huzuni ya msiba huu mkubwa baada ya ule wa kuondokewa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w).
Kumbuka kuwa wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kila sehemu ya dunia wanaomboleza msiba huu wa kifo cha Fatuma Zaharaa (a.s), kunariwaya tofauti kuhusu tarehe ya kifo chake na sehemu lilipo kaburi lake (a.s), hii inaonyesha ukubwa wa dhulma aliyo fanyiwa, iliyo mpelekea atoe usia kwa mume wake kiongozi wa waumini (a.s), afiche sehemu ya kaburi lake na wala jeneza lake lisishuhudiwe na yeyote katika waliomdhulumu haki yake, wakati anafariki alikuwa na umri wa miaka kumi na nane kwa mujibu wa riwaya mashuhuri.