Mawakibu za waombolezaji zimejaa katika barabara za Karbala na kwenye Ataba zake takatifu

Maoni katika picha
Kwa siku ya tatu mfululizo bado mawakibu za waombolezaji kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala zinamiminika katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), wanakuja kuomboleza na kutoa pole kwa kifo cha bibi Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu, na kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya.

Rais wa kitengo hicho bwana Riyadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Maukibu zilizokuja kuhuisha msiba huu zimegawanyika sehemu mbili, sehemu ya kwanza zinatoka ndani ya mkoa wa Karbala na zimekua zikifanya hivyo toka kwenye maombolezo ya kwa mujibu wa riwaya ya pili, na sehemu ya pili ni mawakibu zilizotoka nje ya mkoa, ambapo zinaomboleza siku moja kabla ya tarehe ya kifo chake na zinamaliza tarehe ya kifo chake (a.s)”.

Akabainisha kuwa: “Matembezi ya mawakibu hizo ni utamaduni ulio zoweleka, kipindi hiki huitwa msimu wa huzuni za Fatwimiyya au msimu wa Muharam ndogo, hufanya mambo mbalimbali yanayo ashiria kuomboleza msiba na huendelea na tamaduni hizo hadi baada ya tarehe ya kifo chake, matembezi ya mawakibu hizo huanzia kwenye barabara zinazo elekea kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), huingia hadi ndani ya haram yake takatifu, kisha kutoka na kuelekea kwenye malalo ya Imamu Hussein (a.s) wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu, chini ya utaratibu maalum uliopangwa na kitengo husika, unao endana na mazingira ya sasa, matembezi ya mawakibu hizo yamepangiliwa vizuri kwa namna ambayo hayatatizi harakati za mazuwaru”.

Tambua kuwa hakuna tarehe maalum ya kifo chake (a.s), kuna riwaya tatu tofauti zinazo taja tarehe ya kifo chake (a.s) baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w), hivyo waumini huomboleza kifo chake kwa mujibu wa riwaya zote tatu kila mwaka, na siku za kuomboleza msiba wake huitwa (msimu wa huzuni za Fatwimiyya).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: