Majlisi za kuomboleza: kumbukumbu ya kifo cha Zaharaa (a.s) katika chuo kikuu cha Alkafeel

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya kimeandaa majlisi ya kuomboleza kifo cha pande la damu ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) bibi Fatuma Zaharaa (a.s), ndani ya ukumbi wa chuo hicho na kuhudhuriwa na rais wa chuo Dokta Nurisi Dahani, na wakuu wa idara na vitivo pamoja na wanafunzi.

Majlisi imefunguliwa kwa Quráni tukufu ukafuata mhadhara uliotolewa na Shekh Abdillahi Dujaili, amezungumza nafasi ya bibi Zaharaa (a.s) mbele ya baba yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), hadi akasema: (Fatuma ni pande la damu yangu na mimi na tokana na yeye, atakae muudhi atakua ameniudhi, na mwenye kuniudhi atakua amemuudhi Mwenyezi Mungu), utukufu kama huo hautapatikana kwa mtu mwingine tofauti na Fatuma (a.s) kwa wanaume wala kwa wanawake, akaeleza pia dhulma alizo fanyiwa baada ya kifo cha baba yake (s.a.w.w) na maudhi makubwa aliyo vumilia, ikiwa ni pamoja na kuchomewa nyumba, kuvunjwa mbavu, kuharibu ujauzito wake na kunyimwa nafasi ya kumrithi baba yake pamoja na zawadi aliyopewa na baba yake, na jinsi alivyo pambana na changamoto zote hizo.

Majlisi ikahitimishwa kwa kusoma tenzi za huzuni zinazo amsha hisia za majonzi kwa mambo yaliyo watokea watu wa nyumba ya Mtume (a.s) baada ya kifo chake.

Kumbuka kuwa chuo kikuu cha Alkafeel kimezowea kuadhimisha matukio ya Ahlulbait (a.s) ya tarehe za kuzaliwa na kufariki chini ya utaratibu maalum, na hualika wasomi na wahadhiri mbalimbali katika maadhimidho hayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: