Ufunguzi wa ukumbi wa makumbusho ya Alkafeel baada ya kufanyiwa matengenezo makubwa

Maoni katika picha
Makumbusho ya Alkafeel imefungua milango yake kwa ajili ya kupokea watu wanaokuja kutembelea makumbusho hiyo baada ya ukumbi wa maonyesho kufanyiwa ukarabati mkubwa, na kuwa katika muonekano mpya utakao saidia kutunza malikale zilizopo ambazo historia yake ni ya miongo na miongo.

Rais wa kitengo cha makumbusho Ustadh Swadiq Laazim ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “Hakika kazi ya ukarabati hupewa kipaombele zaidi katika makumbusho, ukiwemo ukarabati wa ukumbi wa maonyesho ya makumbusho ya Alkafeel, tumeandaa ratiba maalum ya ufanyaji wa ukarabati, lakini safari hii tumefanya ukarabati mkubwa zaidi katika sehemu zote za ukumbi, kuanzia sehemu ya kuonyesha mali-kale au mambo mengine”.

Akaongeza kuwa: “Kikosi cha ujenzi na ukarabati kimefanya kazi chini ya mkakati maalum ulio jumuisha mambo yafuatayo:

  • - Kuondoa mazulia (kapeti) za zamani na kutandika mpya zenye randi nzuri na zinazo endana na turathi zilizopo.
  • - Kukarabati sakafu ya ukumbi kwa kuziba sehemu zenye mipafuko na zilizokuwa zimeanza kuharibika.
  • - Kukarabati baadhi ya mali-kale zilizopo katika makumbusho na kuondoa zilizo haribika.
  • - Kubadilisha baadhi ya sehemu zilizokuwa zimewekwa mali-kale na kuwekwa sehemu zingine.
  • - Kusafisha malikale zote chini ya wabobezi wa kazi hiyo na kwa kutumia vifaa maalum.
  • - Kupaka rangi baadhi ya sehemu zilizo kuwa zinahitaji kurudiwa kuwekwa rangi kwenye kabati za maonyesho na kuta.
  • - Ukarabati mkuu wa njia za umeme kuanzia nyaya za umeme na taa za ukumbi wa makumbusho kwa kuondoa sehemu zilizo haribika na kuweka mpya.
  • - Kurekebisha jukwaa kuu la maonyesho.
  • - Kukarabati miswala ya kihistoria iliyopo ndani ya makumbusho”.

Kumbuka kuwa ukumbi wa maonyesho ya makumbusho ya Alkafeel, upo upande wa kulia wa mtu anayeingia kupitia mlango wa Kibla wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), nao ni ukumbi wa kisasa uliojengwa kwa kiwango kikubwa na vifaa vyake vimewekwa katika mpangilio bora zaidi unao saidia kuonyesha mali-kale kwa urahisi sawa na makumbusho zingine za kimataifa, makumbusho inafanya kila uwezale kuhakikisha inaenda pamoja na maendeleo ya dunia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: