Rais wa chuo kikuu cha teknolojia: chuo kikuu cha Alkafeel kinamazingira bora ya kujisomea na rafiki kwa walimu na wanafunzi

Maoni katika picha
Rais wa chuo kikuu cha teknolojia Ustadh Ahmadi Muhammad Hassan Ghabani, amesema kuwa chuo kikuu cha Alkafeel kinastahiki kuitwa jina hilo, kimefanikiwa kuandaa mazingira mazuri ya usomaji kwa walimu na wanafunzi, ambayo wanafaa kuwa katika mazingira hayo bora kwa usomaji.

Ameyasema hayo baada ya kutembelea chuo kikuu cha Alkafeel kilicho chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na kupokewa na rais wa chuo Dokta Nusis Dahani ambaye ametembelea sehemu mbalimbali za chuo hicho, kama vile madarasa, maabara na sehemu zingine za majengo ya chuo, pamoja na kukagua vifaa na njia za ufundishaji sambamba na kusikiliza maelezo kutoka kwa rais wa chuo.

Mwisho wa ziara yake akatoa shukrani nyingi kwa wasimamizi wote na watumishi wa mradi huu wa kielimu, akasema: “Hakika Atabatu Abbasiyya imefanya kazi kubwa katika sekta ya elimu hapa Iraq, inatumia njia sahihi katika miradi yake ya shule, jambo hili sio geni kwa Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akafafanua kuwa: “Ziara hii ni sehemu ya ujumbe wa kujenga ushirikiano wa kielimu baina ya vyuo viwili, utakao saidia vyuo vyote viwili kufikia malengo yake, kwa namna ambayo itaimarisha ushirikiano wa pande mbili na kuanzisha jarida la kielimu la pamoja ambalo nimatumaini yetu litakuwa na matunda mema”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: