(Mbinu za kutatua changamoto).. ndio maudhui ya mhadhara wa mafunzo ya utawala yanayo tolewa na jumuiya ya Skaut ya Alkafeel

Maoni katika picha
Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya idara ya watoto na makuzi katika kitengo cha habari cha Atabatu Abbasiyya, kwenye semina ya utawala na ufuatiliaji inayo tolewa na jumuiya hiyo maudhui ya mada zake inasema (mbinu za kutatua changamoto) kwa lengo la kuongeza uwezo wa washiriki na kuandaa mikakati na kuweka malengo.

Mkufunzi wa semina hiyo Ustadh Maahir Khalidi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Program hii ni sehemu ya ufuatiliaji wa habari unaofanywa na Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel, ambapo jumuiya hutumia kutambua uwezo wa washiriki na kuangalia namna ya kunufaika nao”.

Akaongeza kuwa: “Mhadhara umezungumzia mbinu za kutatua changamoto za kijamii pamoja na aina zake na namna ya kuzibaini, mbinu zilizo fundishwa ni za kisasa, na tumechagua changamoto zinazo wapata vijana kama mfano kwani hilo ndio tatizo kubwa katika jamii”.

Kumbuka kuwa semina inawarsha tofauti, miongoni mwake ni usimamiaji wa jamii na muda pamoja na adabu za kuongea na ufuatiliaji wa kiofisi sambamba na uandishi wa ripoti na uandaaji wa proqram za kuongeza uwezo, washiriki wa semina hiyo ni wanachama wa Skaut tulio wagawa katika makundi kulingana na tofauti za mada.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: