Shule za Al-Ameed zimeanza program kubwa ya kufundisha walimu wa shule za awali zilizo chini yake

Maoni katika picha
Shule za Al-Ameed chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, zimeanza program ya kuwajengea uwezo walimu wake wa shule za awali (chekechea) zilizo chini yake.

Kwa mujibu wa maelezo ya Ustadh Wasim Naafii amesema: “Program inahusisha mbinu bora za ufundishaji hususan katika selebasi ya (Nahwul-Qamar) selibasi maalum ya shule za awali”.

Akaongeza kuwa: “Program hiyo inahusisha pia utoaji wa mafunzo ya mfano kwa lengo la kubadilishana uzowefu na kuongeza uwezo wa kufundisha watoto”.

Akamaliza kwa kusema: “Warsha hii na masomo ya mfano yanayofundishwa kwa watumishi yanalenga kuongeza uwezo wa walimu katika ufundishaji wa watoto, sambamba na hali ambayo taifa linapitia kwa sasa, mazingira ambayo imelazimika kutumia zaidi ufundishaji wa njia ya mtandao, sambamba na kuangalia njia zilizo onyesha mafanikio katika ufundishaji wa watoto, na kuweka mazingira bora kwa watoto”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: