Kumaliza kazi ya kuweka marumaru kwenye eneo la mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimemaliza kazi ya kuweka marumaru kwenye eneo la mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), sehemu inayokadiriwa kuwa na ukubwa wa mita (240), inayo elekea eneo lililowekwa marumaru siku za nyuma hadi mwanzoni mwa sehemu ya haram wake mtakatifu.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh, akaongeza kuwa: “Mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) umeshuhudia ukarabati mwingi, kutokana na umuhimu wa mlango huo, ndio lango kuu na muhimu katika Atabatu Abbasiyya unasifa za pekee tofauti na milango mingine”.

Akaendelea kusema: “Kazi ya kuweka marumaru ni moja ya umaliziaji wa ujenzi na mapambo ya ukuta na dari, katika kazi ya uwekaji wa marumaru kuna mambo yamezingatiwa, ikiwa ni pamoja na urefu wa mlango upande wa kuingia na upande wa haram tukufu, kwa namna ambayo hautatizi harakati za mazuwaru na mawakibu, tumetumia vifaa bora na imara pamoja na mfumo mzuri wa uwekaji wake, aina tuliyo tumia inafanana na zilizo tumika kwenye milango mingine”.

Kumbuka kuwa mradi wa mlango ni miongoni mwa miradi mikubwa ya upanuzi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, mlango mpya umekua mkubwa zaidi ya mlango wa kwanza, na umewekwa mapambo na nakshi nzuri za kiislamu.

Milango hiyo imesanifiwa na kutengenezwa na shirika la ardhi takatifu la ujenzi, chini ya usimamizi wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, milango hiyo imetengenezwa kwa umaridadi na weledi wa hali ya juu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: