Ofisi ya Marjaa Dini mkuu imelaani milipuko ya kikaidi iliyo tokea katika uwanja wa ndege

Maoni katika picha
Ofisi ya Marjaa Dini mkuu siku ya Alkhamisi (7 Jamadal-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (21 Januari 2021m) imelaani milipuko ya kigaidi lililotokea katika uwanja wa ndege.

Lifuatalo ni tamko la kulaani lililosambazwa na toghuti ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Ayatullah Sayyid Sistani:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.

(Sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea)

Kwa mara nyingine magaidi wamewalenga wananchi kwa kulipua uwanja wa ndege wa Bagdad, na kuuwawa kishahidi makumi ya watu na wengine wengi kujeruhiwa, katika hali ya kuhuzunisha na kuumiza kila mwenye roho ya ubinaadamu.

Tunatoa pole kwa familia za mashahidi watukufu na tunamuomba Mwenyezi Mungu awaponye haraka majeruhi, tunaviomba vyombo vya ulinzi na usalama viimarishe ulinzi na kufanya uchunguzi wa kina kuwabaini magaidi wanaoendeleza maafa kwa raia wa taifa hili, hakuna hila wala nguvu ispokua kutoka kwa Mwenyezi Mungu mkuu.

7/ Jamadal-Aakhar/ 1442h.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: