Kituo cha turathi za Karbala kinapokea mwaka wa 2021m kwa kufanya nadwa ya kitafiti kuhusu turathi za Allamah Jafari Twabatwabai

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinapokea mwaka mpya kwa kufanya nadwa ya kitafiti yenye anuani isemayo: (Turathi za Alamah Mirza Jafari bun Ali Naqiy Twabatwabai Alhaairiy) kwa ajili ya kuangazia turathi zake za nakala-kale (makhtuutu), asubuhi ya Ijumaa mwezi (8 Jamadal-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (22 Januari 2021m) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) na kuhudhuriwa na kundi la wasomi wa mambo ya turathi, pamoja na wawakilishi wa uongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na vitengo vyake, vyombo vingi vya habari vimeripoti nadwa hiyo.

Nadwa imefunguliwa kwa Quráni tukufu ukafuata ujumbe wa kituo cha turathi za Karbala ulio wasilishwa na Dokta Ihsaan Ali Gharifi, akasema: “Hakika juhudi za kituo cha Karbala katika kuhuisha turathi za nakala-kale ni moja ya mkakati mkuu wa baadae, inafanyika bidii kubwa ya kuutekeleza na kuonyesha turathi tukufu za mji wa Imamu Hussein (a.s), kwa ajili hiyo tumeanza kuhakiki nakala-kale na ujumbe ambao ni hazina ya kielimu kwa wanachuoni wa mji wa Karbala”.

Baada ya hapo vikaanza vikao vya kuwasilisha mada za kitafiti chini ya usimamizi wa Dokta Ali Twahir Alhilliy kama ifuatavyo:

Mada ya kwanza inasema: (Ujumbe wa Allamah Mirza Jafari Twabatwabai Al-Haairiy) mtoa mada ni Sayyid Muhammad Jaasim Almussawi.

Mada ya pili inasema: (Utafiti katika ujumbe wa mafanikio ya mgonjwa wa Mirza Jafari Twabatwabai Alhaairiy) mtoa mada ni Shekh Muhammad Dhwalimi.

Mada ya tatu inasema: (Utafiti katika ujumbe wa safari ya Mirza Jafari Twabatwabai Alhaairiy) mtoa mada ni Shekh Jaasim Silawi.

Mata ya nne inasema: (Utafiti katika ujumbe wa talaka ya mgonjwa uliofanywa na Mirza Jafari Twabatwabai Alhaairiy) mtoa mada ni Shekh Ahmadi Hamidawi Mussawi.

Mjadala ulikua wazi wakati wote wa kikao, wahudhuriaji wamejadiliana na watoa mada moja kwa moja, majadiliano yalikua mazuri pamoja na maoni mbalimbali, washiriki wamepongeza malengo ya nadwa na mada zilizo wasilishwa, wametoa shukrani nyingi kwa uongozi wa kituo cha turathi za Karbala kwa program hii, wameomba kuendelea zaidi kufichua turathi za mji wa bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: