Jumuiya ya Al-Ameed inajadili mambo mbalimbali kuhusu miradi yake

Maoni katika picha
Wajumbe wa kamati kuu ya jumuiya ya Al-Ameed, wamejadili mambo mbalimbali kuhusu miradi yake, katika kikao kilicho ongozwa na rais wake Sayyid Liith Mussawi kilicho fanyika ndani ya Ataba takatifu, asubuhi ya Ijumaa mwezi (8 Jamadal-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (22 Januari 2021m).

Huu ni mkutano wa kwanza katika mwaka, yamezungumzwa mambo yanayo husiana na malengo ya kuanzishwa kwa jumuiya hii, pamoja na mipango ya baadae na miradi inayo tarajiwa kufanywa, pamoja na kuweka mpango kazi wa mambo muhimu yatakayo fanywa, sambamba na kujadili maoni mbalimbali yanayohusu vitengo vya jumuiya.

Hali kadhalika kikao kimejadili mambo tofauti yaliyo wasilishwa na wajumbe wa kamati, ikiwa ni pamoja na kualika wataalam wa fani mbalimbali zinazo hitajiwa na jumuiya kielimu na kitamaduni.

Mwisho wa mkutano Mheshimiwa Sayyid Liith amewashukuru wajumbe kwa kazi kubwa waliyo fanya katika mkutano huu, na kuwataka wapange mkutano mwingine kwa ajili ya kujadili utekelezaji wa mambo waliyokubaliana kwenye huu mkutano.

Kumbuka kuwa jumuiya ya Al-Ameed ya kielimu na kitamaduni imesajiliwa na wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu, chini ya amri ya wizara namba 2 – 7199 tarehe 24/7/2019m.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: