Ugeni kutoka idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na shule umetembelea idara ya malezi ya mkoa wa Muthanna kujadili njia za kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja

Maoni katika picha
Mkuu wa idara ya malezi katika mkoa wa Muthanna Ustadh Saadi Khadhar Abbasi amepokea ugeni kutoka idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na shule chini ya kitengo kikuu cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya, chini ya uongozi wa Ustadh Maahir Khalidi, kujadili njia za kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja, kwa ajili ya kutumikia sekta ya malezi na elimu hapa mkoani.

Tumeongea na kiongozi wa ujumbe huo Ustadh Mahmuud Qarah Ghuli amesema kuwa: “Idara imechukua jukumu la kufanya mambo kadhaa na baadhi ya mambo imewaachia wanafunzi na walimu pamoja na viongozi wa vituo vya malezi hapa mkoani, ziara hii imefanywa kwa ajili ya kuangalia namna ya kushirikiana, kiongozi wa kituo cha malezi cha Muthanna amefanya makubaliano maalum ya kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu, sambamba na kuendesha miradi ya wanafunzi na walimu, au kuwaandalia semina kutokana na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa, akasisitiza kuwa Atabatu Abbasiyya ilikuwa na inaendelea kua msaigizi mkuu katika sekta ya malezi na elimu”.

Akaongeza kuwa: “Ustadh Maahir amesema kuhusu ratiba inayotumiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara, na malengo wanayo kusudia kutatimiza, kama vile safari za kielimu na masomo ya kitamaduni pamoja na semina mbalimbali”.

Akabainisha kuwa: “Mwisho wa kikao baada ya kuongelewa mambo mbalimbali mkuu wa kitengo amepongeza mambo yaliyo kubaliwa na kuanza kufanyiwa kazi, lakini akatanabahisha kuwa siku za mbele kutakua na haja ya kuimarisha pamoja na ulazima wa kufanya kazi kwa mpangilio, na kuwa na makongamano ya pamoja ya kujadili hali ya malezi na elimu hapa mkoani”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: