Kazi ya kutengeneza dirisha la Maqaam ya mkono wa kushoto wa Abulfadhil Abbasi (a.s) imefika hatua kubwa

Maoni katika picha
Kazi ya kutengeneza dirisha la Maqaam ya mkono wa kushoto wa Abulfadhil Abbasi (a.s) imepiga hatua kubwa, sehemu nyingi zipo katika hatua ya mwisho, kazi ya kukamilisha sehemu zilizo baki bado inaendelea kama ilivyo pangwa na kitengo cha utengenezaji wa madirisha ya makaburi na milango mitakatifu chini ya Atabatu Abbasiyya, kwa ajili ya kukamilisha ndani ya muda uliopangwa, bila kuharibu utendaji wa kazi zingine, kama vile utengenezaji wa dirisha la Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) na dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s), kazi zote zinaendelea vizuri na zinatarajiwa kukamilika ndani ya muda uliopangwa na kwa ubora unaotakiwa.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo hicho Sayyid Naadhim Ghurabi, akaongeza kuwa: “Hakika dirisha la Maqaam ya mkono limeshuhudia maendeleo makubwa, sehemu zote za madirisha zimekamilika, jumla zipo sehemu nane, zina urefu wa (sm 190) na upana wa (mt 1), kunaviduara (176) na mapambo (42) yaliyogawanywa mara mbili (21) pamoja na sehemu iliyowekwa nakshi za mimea zinazo fanana na zile zilizopo kwenye dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), yamewekwa kwa mfano wa chuma chenye umbo la namba nane”.

Akaongeza kuwa: “Hali kadhalika tumemaliza kutengeneza nguzo za msingi zipatazo (8) zinazo zunguka dirisha na zenye mapambo ya nakshi za mimea, pia tumemaliza utengenezaji wa sehemu za vitako vya nguzo hizo vipatavyo (16) ambavyo vinamapambo ya (taji za nguzo)”.

Akaendelea kusema: “Kazi inayo endelea kwa sasa ni kuweka mapambo ya mwisho kwenye ufito wenye maandishi ya shairi unaozunguka dirisha, kila sehemu inatenganishwa na pambo la uwa pamoja na pambo lingine linalo kuwa sawa na kitu kimoja”.

Akabainisha kuwa: “Ndani ya dirisha kumewekwa mbao ya Swaaghi iliyo nakshiwa na kuwekwa mapambo ya rangi tofauti, uimara wake hautofautiaji na upande wa nje, kazi hiyo pia imeshakamilika”.

Kumbuka kuwa dirisha la pande nane ndio la kwanza kutengenezwa katika muundo huo, mzunguko wake ni (mt 3) na urefu wake (mt 2.85) umbo lake limewekwa silva ya ujazo wa (ml 2), limesanifiwa na kutengenezwa kwa weledi na ubora mkubwa, kazi hii imeingizwa katika orodha ya mafanikio yaliyofanywa na kamati hiyo ndani na nje ya Iraq, yanayotokana na kazi zinazo fanywa na mikono ya raia wa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: