Ugeni kutoka Ataba mbili takatifu unatoa pole kwa familia za mashahidi wa mripuko wa uwanja wa ndege

Maoni katika picha
Ugeni kutoka Ataba mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya umetoa pole kwa familia za mashahidi wa shambulio ya kikaidi lililotokea uwanja wa ndege jijini Bagdad, siku ya Alkhamisi ya mwezi (7 Jamadal-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (21 Januari 2021m).

Ugeni huo umejumuisha viongozi wa Ataba mbili takatifu na watumishi wake, umefikisha salamu kutoka kwa Marjaa Dini mkuu na viongozi wake wakuu wa kisheria pamoja na watumishi wa malalo mbili takatifu kwa familia za mashahidi hao.

Muwakilishi wa Atabatu Abbasiyya katika ugeni huo na rais wa kitengo cha Dini Shekh Aadil Wakiil amesema kuwa: “Kutokana na maelekezo ya wakuu wa kisheria katika Ataba mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya tumekuja kushiriki vikao vya uombolezaji wa mashahidi wapenzi walio uwawa kwenye shambulio la kigaidi lililotokea uwanja wa ndege, na kuwafanya watukufu hawa kuingia katika orodha ya mashahidi wa Iraq”.

Familia za mashahidi zimeshukuru sana ujio wa ugeni huo.

Kumbuka kuwa ofisi ya Marjaa Dini mkuu ilitoa tamko la kulaani shambulio hilo, pamoja na kutoa pole kwa familia za mashahidi na kuwaombea dua majeruhi wapone haraka, sambamba na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuimarisha ulinzi na kutibua njama za magaidi wanaoshambulia raia watukufu wa taifa hili lenye changamoto nyingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: