Maandalizi ya shindano la Fatwimiyya kwa wanawake litakalo fanyika kwa njia ya mtandao na mubashara

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya chini ya ofisi ya katibu mkuu katika Atabatu Abbasiyya tukufu Asubuhi ya Jumapili mwezi (10 Jamadal-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (24 Januari 2021m) inaandaa shindano la Fatwimiyya kwa ajili ya wanawake tu, kama sehemu ya kuomboleza kifo cha bibi Fatuma Zaharaa (a.s), na kuenzi mafundisho yake kupitua khutuba aliyotoa kwa wanawake wa Muhajirina na Answaru walipo kwenda kumtembelea.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara hiyo bibi Taghridi Tamimi amesema: “Shindano litafanyika mubashara ndani ya Sardabu ya Imamu Ali Haadi (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu na chuo kikuu cha Alghadiir katika mkoa wa Najafu, kwa kufuata maelekezo yote ya kujikinga na maambuzi na kuhakikisha usalama wa washiriki, hususan kwa washiriki wanaotoka nje ya Iraq na wale walioshidwa kuhudhuria kutokana na umbali wa sehemu wanazo ishi, wamepewa nafasi ya kushiriki moja kwa moja kwa kutumia mitandao ya mawasiliano ya kijamii:”.

Akaongeza kuwa: “Maswali ya shindano yanalenga kuhifadhi maana ishirini katika maana za maneno ya khutuba, na kuandika nakala ya khutuba pamoja na kuchagua majibu sahihi kwenye maswali matano yanayo tokana na nakala ya khutuba, majibu yote ya washiriki yatawasilishwa kwenye kamati ya majaji kwa ajili ya kusahihishwa na kupiga kura ili kupata mshindi mmoja iwapo kukiwa na washindi wengi katika nafasi moja, kutakuwa na zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa kumi”.

Kumbuka kuwa idara ya wahadhiri inautaratibu wa kuandaa mashindano kutokana na matukio ya mwaka, miongoni mwa mashindano hayo ni hili la kukumbuka kifo cha bibi Fatuma Zaharaa (a.s), na imechaguliwa khutuba hii kushindaniwa kwa sababu inamafundisho ya kifiqhi, kiaqida na kiakhlaqi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: