Zaidi ya watu milioni moja wamefanyiwa ziara kwa niaba ndani ya mwaka 2020m

Maoni katika picha
Idara ya taaluma na teknolojia chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu imesema kuwa, dirisha la ziara kwa niaba lililopo katika mtandao wa kimataifa Alkafeel, imepokea maombi ya ziara na kufanya zaidi ya ziara milioni moja na laki moja na elfu sitini na nane mia sita na nane (1,168,608) kutoka nchi tofauti duniani, kupitia mitandao yake ya (kiarabu – kiingereza – Kiswahili – kijerumani – kifarsi – kituruki – kiurdu - kifaransa).

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara hiyo Ustadh Haidari Twalibu Abdul-Amiir, akaongeza kuwa: “Kutokana na mazingira ambayo dunia imepitia mwaka jana likiwemo taifa la Iraq, mazingira ya maambukizi ya virusi vya Korona yaliyo sababisha idadi kubwa ya watu kushindwa kuja kufanya ziara kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na malalo zingine za Maimamu (a.s) ndani na nje ya Iraq, hivyo dirisha la ziara kwa niaba limeshuhudia ongezeko kubwa la watu waliojisajili kutoka nchi tofauti duniani tofauti na idadi ya watu waliojisajili mwaka uliopita”.

Akafafanua kuwa: “Hivyo tuliweka utaratibu maalum wa kuwafanyia ziara kwa niaba, kazi hiyo imefanywa na Masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ibada hiyo imefanyiwa ndani ya malalo takatifu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) huku ziara zingine zikifanyiwa kwenye malalo za wahusika ndani na nje ya Iraq, kila sehemu kuna watu wamejitolea kufanya ibada ya ziara kwa niaba kulingana na tukio pamoja na ratiba iliyopangwa, ikiwa ni pamoja na malalo ya Imamu Ali (a.s) katika mji wa Najafu, malalo ya Maimamu wawili Aljawadaini katika mji wa Bagdad na Askariyyaini katika mji wa Samaraa, pamoja na ziara ya bibi Zaharaa (a.s) na Maimamu waliozikwa Baqii (a.s) katika mji wa Madina, na bibi Zainabu (a.s) nchini Sirya, na Imamu Ridhwaa pamoja na dada yake Sayyidat Maasuma (a.s) nchini Iran”.

Akamaliza kwa kusema: “Tulitoa muda mrefu wa kutangaza ziara hizo kabla ya tukio husika, ili tuweze kupokea idadi kubwa zaidi ya wasajiliwa, asilimia kubwa wametoka katika nchi zifyatazo: (Iraq, Iran, Lebanon, Pakistani, Urusi, Marekani, Uingereza, India, Saudia, Swiden, Kanada, Kuwait, Malezia, Australia, Aljeria, Baharain, Misri, Ujerumani, Island, Namsa, Yunani, Holand, Tunisia, Denmak, Norwey, Qatar, Ubelgiji, Moroko, Afghanistani, Omani, Ekowado, Brazili, Ajentina, Uswisi, Naijeria, Ghana, Yemen, Indonesia, Italia, Hispania, Ufaransa, Uturuki, Adharbaijani, Qabrus, Finland, China, Ailend, Honkon, Japani, Falme za kiarabu, Sudani)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: