Ugeni kutoka Ataba mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya unatembelea watu waliojeruhiwa katika mripuko wa uwanja wa ndege

Maoni katika picha
Ugeni kutoka Ataba mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya umetembelea watu waliojeruhiwa katika shambulizi la kigaidi lililo tokea uwanja wa ndege wa Bagdad siku ya Alkhamisi (7 Jamadal-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (21 Januari 2020m) waliolazwa katika hospitali ya rufaa ya Bagdad, baada ya kutoa rambirambi kwa familia za mashahidi wa shambulio hilo.

Muwakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika ugeni huo Shekh Aadil Wakili ameongea na mtandao wa Alkafeel kuhusu ziara hiyo kuwa: “Ndani ya siku mbili mfululizo, ugeni kutoka Ataba mbili takatifu umetembelea familia za mashahidi wa shambulio la kigaidi lililofanywa na watu wanaotaka kuangamiza taifa hili na raia wake watukufu, tumefikisha rambirambi za viongozi wawili wakuu wa kisheria kutoka Ataba mbili takatifu pamoja na watumishi wao, baada ya kumaliza jaula hiyo iliyo tufikisha katika vitongoji tofauti vya mji mkuu wa Bagdad, tulikwenda katika hospitali ambayo majeruhi wa shamulio hilo wamelazwa na kuangalia hali ya afya zao, na kuwaombea wapone haraka pamoja na kuwafikishia salamu za watumishi wa Ataba mbili takatifu na dua zao, na tukawapa zawadi za kutabaruku kutoka katika malalo ya Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na zawadi zingine”.

Majeruhi na familia zao wamepongeza ziara hiyo iliyofanywa na ugeni wa Ataba mbili takatifu kwa ajili ya kuwajulia hali, na wakauomba ugeni uwafikishie shukrani na salamu zao kwa viongozi wakuu wa Ataba mbili takatifu kutokana na moyo wa ubinaadamu walio onyesha kwao.

Kumbuka kuwa ofisi ya Marjaa Dini mkuu ilitoa tamko la kulaani shambulio hilo, pamoja na kutoa pole kwa familia za mashahidi na kuwaombea dua majeruhi wapone haraka, sambamba na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuimarisha ulinzi na kutibua njama za magaidi wanaoshambulia raia watukufu wa taifa hili lenye changamoto nyingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: