Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara Shekh Abdu-Swahibu Twaaiy amesema kuwa: “Ni moja ya majlisi itakayo simamiwa na idara kwa ajili ya kuhuisha tukio muhimu lililopo ndani ya ratiba ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na majlisi hiyo ipo ndani ya mradi wa Ummul-Banina (a.s) unao husika na (kuhuisha matukio ya kidini ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi –a.s-)”.
Akaongeza kuwa: “Majlisi itadumu kwa muda wa siku tatu, kuanzia mwezi (11 Jamadal-Aakhar) kila siku kutakua na mihadhara miwili, mhadhara wa kwanza utatolewa asubuhi na Sayyid Hashim Husseini na wa pili jioni utatolewa na Shekh Ahmadi Rabii, na atashiriki muimbaji bwana Baasim Karbalai kusoma matam”.
Tambua kuwa ratiba ya kuomboleza iliyo andaliwa inavipengele vifuatavyo:
- - Kufanya majlisi za kuomboleza asubuhi na jioni ndani ya siku tatu katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) chini ya usimamizi wa idara ya wahadhiri wa Husseiniyya.
- - Muhadhara wa kidini utakao tolewa na kitengo cha Dini siku ya kumbukumbu ya kifo.
- - Kuratibu majlisi za wanawake ndani ya sardabu ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
- - Kuratibu majlisi ya kuomboleza ya masayyidi wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya.
- - Kuweka utaratibu wa kupokea mawakibu za waombolezaji kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, chini ya usimamizi wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili takatifu.
- - Kufungua mlango wa usajili wa ziara ya Ummul-Banina (a.s) kwa niaba kupitia dirisha la ziara kwa niaba katika mtandao wa kimataifa Alkafeel.
- - Kuweka mapambo meusi katika haram tukufu.
- - Kitengo cha mgahawa (mudhifu) kugawa mamia ya sahani za chakula kwa mazuwaru na waombolezaji.