Chuo kikuu cha Alkafeel kinafanya nadwa ya kielimu kujadili chanjo ya Korona

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya nadwa ya kielimu kujadili chanjo ya Korona, nadwa hiyo imefanywa baada ya mashirika ya kutengeneza dawa kutangaza kuwa yamefanikiwa kutengeneza chanjo hiyo.

Dokta Shaakir Jawaad aliyekuwa kiongozi wa idara ya afya ya kimataifa na taasisi ya Henry-Jokson ambaye pia ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Jomaison nchini Marekani ndiye mtoa mada katika nadwa hiyo, iliyo endeshwa kwa njia ya (zoom), na kufatiliwa na wadau wengi wa sekta ya afya wakiwemo wahadhiri wa vyuo vikuu.

Amezungumza mambo mengi katika mhadhara wake, kama vile chanzo cha virusi vya Korona na chanjo dhaifu au zisizokua dhaifu, na njia za matibabu (tiba zinazo saidia – dawa zinazoweza kupambana na virusi – dawa zinazo weza kuondoa madhara) hali kadhalika ameeleza hatua walizopitia katika uandaaji wa chanjo hiyo, ambapo walianza kufanya utafiti wa kina kabla ya kufanya (majaribio kwa wanyama).

Kisha wakaingia katika hatua ya utafiti kwa binaadamu.

Nadwa imepanbwa na maoni pamoja na maswali kutoka kwa washiriki kuhusu chanjo hiyo na namna ya matumizi yake, mwisho wa nadwa Dokta Shaakir amesisitiza umuhimu wa kutumia chanjo kama inavyo elekezwa na taasisi za afya za kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: