Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea na ratiba ya kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s)

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika siku ya pili ya ratiba yake ya kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha Ummul-Banina (a.s), umefanya majlisi ya kuomboleza ndani ya haram jioni ya siku ya Jumanne mwezi (12 Jamadal-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (26 Januari 2021m).

Majlisi imefunguliwa kwa Quráni tukufu ukafuata Mhadhara wa kidini uliutolewa na Shekh Ahmadi Rabii, ameeleza historia tukufu ya Ummul-Banina (a.s) na heshima kubwa aliyonayo mbele ya mume wake kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), akafafanua pia mchango wake katika vita ya Twafu pale alipowatoa watoto wake wanne kwenda kumtetea bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s) wakiongozwa na mwezi wa Bani Hashim Abulfadhil Abbasi (a.s).

Baada ya hapo muimbaji wa Husseiniyya bwana Baasim Karbalai akapanda mimbari na kusoma kaswida zilizo eleza ukubwa wa msiba huo na huzuni waliyonayo waumini.

Kumbuka kuwa mwezi kumi na tatu mwaka wa (64h) alifariki mama mtukufu Ummul-Banina aliyekuwa mke wa kiongozi wa waumini (a.s), aitwae Fatuma bint Hizaam Alkilabiyya Al-Aamiriyya, alipewa jina la Umuul-Banina kwa sababu alikuwa na watoto wanne wa kiume waliokufa katika vita ya Twafu huko Karbala kwa ajili ya kumnusuru bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s), alifia Madina na akazikwa katika makaburi ya Baqii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: