Kumbukumbu ya kifo cha bibi wa uaminifu na chemchem ya utukufu na kujitolea Ummul-Banina (a.s)

Maoni katika picha
Siku kama ya leo mwezi kumi na tatu Jamadal-Aakhar tunakumbuka kifo cha bibi mtukufu Ummul-Banina (a.s), jina lake ni Fatuma mtoto wa Hizaam mtoto wa Khalidi mtoto wa Rabia Alkilabi, alizaliwa mwaka wa tano Hijiriyya kwa mujibu wa riwaya mashuhuri, akaolewa na kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), na watoto wake ni Abbasi Abulfadhil, Abdullahi, Jafari, Othumani, wote waliuwawa chini ya bendera ya Immamu Hussein (a.s) katika ardhi ya Karbala.

Ummul-Banina (a.s) aliwalea wajukuu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na mabwana wa vijana wa peponi Hassan na Hussein (a.s), aliwaonyesha mapenzi na upole wa hali ya juu kwa namna ambayo aliweza kuwa mbadala bora wa kumkosa mama yao mbora wa wanawake wa duniani, alifariki (a.s) akiwa na umri mdogo na akaacha huzini kubwa katika nafsi za wapenzi wake.

Hakika Ummul-Banina (a.s) aliwapa kipaombele watoto wa Mtume (s.a.w.w) kushinda watoto wake, historia haijaripoti mwanamke aliyewapenda zaidi watoto wa mume wake na akajitolea watoto wake kwa ajili ya kulinda watoto wa mume wake zaidi ya mama huyu mtakatifu, alifanya hivyo kama wajibu wa kidini kwake kwani Mwenyezi Mungu ameamuru kuwapenda wajukuu wa Mtume wake ndani ya Quráni tukufu, alitambua vyema jambo hilo na kulifanyia kazi kwa kuwapa huduma bora zaidi.

Baada ya kumhudumia bwana wa mawasii (a.s) na watoto wake Maimamu watakatifu (a.s) na wajukuu wa Mtume (s.a.w.w) mabwana wa vijana wa peponi, pamoja na kumhudumia Aqiilatu bani Hashim Zainabu Kubra (a.s) baada ya umri alioishi (a.s) baina ya ibada na huzuni ndefu ya kuwakosa mawalii wa Mwenyezi Mungu mtukufu, pamoja na maumivu makali ya kifo cha Imamu Ali bun Abu Twalib katika mihrabu, na kuuwawa watoto wake wanne wakati mmoja kwa ajili ya kumlinda mjukuu wa Mtume Imamu Hussein (a.s), baada hayo yote akafariki mwezi kumi na tatu Jamadal-Aakhar mwaka wa (64h) na kwenda kwa Mola wake mtukufu.

Amezikwa katika makaburi ya Baqii, karibu na kaburi la Ibrahim, Zainabu, Ummu-Kulthum, Abdullahi, Qassim pamoja na maswahaba wengine na mashahidi, kaburi lake lilibomolewa pamoja na makaburi ya Maimamu na watu wa nyumba ya Mtume (a.s).

Amani iwe juu mwanamke huyu mwema mtakasifu, aliye muwakilisha Zaharaa katika msiba wa Hussein (a.s) na akafanya vikao vya kuomboleza msiba huo, hongora kwake na kwa kila aliye fuata nyayo zake, amani iwe juu yake siku aliyozaliwa na siku aliyokufa na siku atakayo fufuliwa hai kwa idhini ya Mola wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: